Kwenye maisha tunayoishi kuna
mambo mbali mbali tunakutana nayo. Tunakumbana na matatizo ya maisha, tunapata
changamoto za maisha. Vile vile tunapata mafanikio ya maisha. Watu tunakuwa na
furaha tunapopata mafanikio. Lakini tukija upande wa pili huwa tunapatwa na
huzuni tunapoyakosa mafanikio. Kwenye maisha ya kila siku kuna makosa mbali
mbali ambayo watu wanakuwa wanayarudia. Makosa hayo yanapelekea kugharimu
mafanikio yao kwenye maisha.
Haya hapa ni makosa 4 ambayo
watu wanayafanya:
1.
Kufanya Vitu Ambavyo huvipendi
Hakuna kosa baya kwenye maisha
tunayoyaishi kama kufanya mambo ambayo huyapendi. Tumeona watu wengi wamezoeya
kufanya kazi wasizozipenda. Wanafunzi wanasoma kozi ambazo hawazipendi, na watu
wanafanya mahusiano na watu wasiowapenda. Matokeo yake ni kupata matatizo
ambayo yanakuwa ni gharama kwenye maisha. Unapoamua kuachana na vitu
usivyovipenda utajikuta unatumia muda wako vizuri. Unatumia nguvu zako
nyingi kwenye shughuli zenye maana kwako na maisha yako.
2.
Kuishi Kwa Kufikiria Mambo
Yaliyopita
Tunapoteza muda wetu mwingi kwa
kufikiria makosa tuliyoyafanya nyuma. Mambo yaliyopita yamepita hatuna ujanja
wa kuyarudisha tena. Kuendelea kufikiria makosa ambayo umeshayafanya nyuma
kunaweza kukusababishia kurudi nyuma kwenye maisha. Epukana na mawazo ya nyuma
badala yake weka juhudi kwenye kile unachokifanya kwa sasa.
3.
Hatuziendei Ndoto Zetu
Hili ni kosa jengine
tunalolifanya kila siku kwenye maisha yetu. Watu wengi wanakuwa na mambo mengi
yasiyo ya msingi kwenye vichwa vyao. Watu wanakuwa na tabia ya kutaka kufanya
kila kitu kinachokuja mbele yake. Matokeo yake wanashindwa njiani kwa sababu
amefanya kitu ambacho hakihusiani na ndoto yake.
4.
Hatuna Mipango
Maisha tunayoishi yanahitaji
malengo na mipango. Tunahitaji kupanga maisha yetu ya kila siku, wiki, mwezi na
hata mwaka. Maisha bila mipango ni kosa kubwa linalopelekea kufeli kwenye
maisha yetu. Kama hatupendi kufanya kosa hili basi njia mzuri ya kufanya ni
kuandika mipango yetu. Mipango inayoelezea kila hatua tunayotaka
kuifikia.
Epuka makosa haya ambayo watu
wengi wamekuwa wakiyarudia rudia kila siku. Na kosa kubwa ambalo huwa
tunalifanya ni lile la kurudia rudia makosa ambayo tunaendelea kuyafanya.
Waswahili wanasema kufanya kosa sio kosa kosa ni kurudia kosa. Hivyo ushauri
wangu kwenye makala hii ni kukusihi usirudie makosa.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena