Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Makosa 9 Ambayo Wamiliki Wengi Wa Biashara Wamekuwa Wakiyarudia Rudia Na Kuwagharimu Kwenye Biashara Zao.


Unapoingia kwenye biashara unatakiwa uwe makini ili kuweza kutengeneza faida ya biashara. Wafanyabiashara wengi wamekosa uwezo wa kuongoza biashara zao ili ziweze kuwapatia mafanikio. Na hii inatokana na makosa wanayoyafanya kila siku kwenye biashara zao.

Yafuatayo  ni makosa 9 ambayo wamiliki wa biashara wanayafanya kwenye biashara zao:
1.           Kukosa Lengo Linaloeleweka
Mfanyabiashara lazima awe na muda wa kutosha wa kutengeneza dira na mtazamo wa biashara anayoifanya. Ni muhimu kufanya hivyo kwenye biashara yoyote ile unayotaka kuifanya. Biashara inahitaji maelezo yanayoelezea kwa nini inatakiwa kuwepo. Biashara ambayo imekosa malengo yanayoeleweka ni rahisi kufeli.
2.           Kukosa Mipango
Wafanyabiashara wengi wanakosa mipango mizuri katika kuendesha biashara zao. Biashara lazima iwe na mipango. Haijalishi kama ni biashara ndogo au kubwa. Ukishindwa kupanga kwenye biashara unayoifanya basi unakaribisha kushindwa.
3.           Kukosa Bajeti
Huwezi kuendesha biashara pasipo kuwa na bajeti ya biashara. Ili kuweza kuona faida ya biashara ni muhimu kuandaa bajeti ya mwaka. Hii itakusaidia kufuatilia mipango na malengo ya biashara. Biashara nyingi zinakufa kila siku kwa sababu zinaendeshwa bila ya bajeti.

4.           Kukosa Wafanyakazi Wanaoweza Kuwajibika
Biashara ambayo itakosa wafanyakazi ambao sio wawajibikaji kwenye kazi zao ni vigumu biashara kuendelea. Biashara ambayo inalipa mishahara lakini haitimizi malengo yake haiwezi kufanikiwa. Kuwaongoza wafanyakazi katika kufuatilia utendaji wao kutakusaidia usifanye makosa yanayoweza kujirudia katika biashara.

5.           Huendani Na Mabadiliko Ya Soko
Kwenye biashara mabadiliko ya soko hutokea mara kwa mara. Ni muhimu kuangalia soko linaendaje ili biashara yako iendane na mabadiliko hayo. Soko linaweza kuhusisha na mabadiliko ya teknolojia au mahitaji ya wateja.

6.           Huwafahamu Wateja
Ni muhimu kuwafahamu wateja wako wanahitaji nini.  Wateja ndio wanaoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara yako. Biashara inaweza kuanguka au kusimama kutokana na wateja. Hivyo jenga ukaribu na wateja . Kufanya hivyo kutakusaidia usifanye kosa hili la kutowafahamu wateja ambao wanaweza kuangusha biashara yako.

7.           Humjali Mfanyakazi Wako
Mfanyakazi wako ndiye mteja wa kwanza katika biashara yako. Mpatie mfanyakazi wako mafunzo ya kutosha yanayoendana na biashara yako. Fuatilia kwa ukaribu maendeleo yake . Anapofanya vizuri mpongeze kwa zawadi. Mfanyakazi anayeongozwa vizuri  lazima awe na furaha. Furaha yake ni matunda mazuri katika uzalishaji wa biashara.

8.           Kukosa Mawasiliano Mazuri
Mawasiliano mabaya ni sumu kwenye biashara zilizo nyingi. Biashara yenye mafanikio inatengeneza mtandao mzuri wa mawasiliano baina ya mteja na mfanyakazi.

9.           Huangalii Njia Za Kuboresha
Biashara yenye mafanikio huangalia njia za uboreshaji wa huduma inazotoa. Mmiliki wa biashara ana wajibu wa kuangalia njia za kuboresha huduma kwa wateja wake. Biashara ambayo haina mpango wa uboreshaji huduma ni rahisi kufeli.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA