Jumapili, 23 Oktoba 2016

Siri Moja Ya Kufanikiwa Kimaisha Ni Kuanza


Kazi ngumu ya kukamilisha kila kitu ni kuanza. Katika maisha hakuna jambo gumu kama kuishawishi akili  yako ili  iweze kuanza. Lakini mara unapoanza unakuwa tayari umefungua milango ya kukamilisha. Kwenye kazi zetu na kwenye biashara tunakuwa na shauku kutekeleza malengo makubwa, lakini tunapokuja kwenye suala la utekelezaji tunakuwa tunasumbuliwa na jinamizi la kuanza.


Kama utaangalia watu walio wengi walioweza kufanikiwa walikuwa na kila sababu ya mafanikio kutokana na kuweza kugundua siri hii ya mafanikio.

Watu Waliofanikiwa Waliweza Kuanza.
Ukiwa utachunguza tabia za watu waliofanikiwa basi tunaweza kusema waliofanikiwa waliweza kuthubutu kuanza kabla hawajawa tayari kuanza. Tambua kwamba hakuna siri nyengine. Hakuna kitu maalumu ambacho watu waliofanikiwa wamezaliwa nacho lakini ambao wameshindwa kufanikiwa hawana. Wao kwao ilikuwa ni kazi rahisi kuweza kuwa na msukumo wa kuanza kufanya kitu kipya.

Kitu Kibaya Zaidi Ambacho Kinaweza Kukutokea.
Moja ya hofu yetu kubwa ni kuonekana kuwa tumeshindwa. Tumekuwa na hofu kufeli zaidi kuliko kuonekana tunafeli. Ndio maana watu wengi kabla ya hata kusubiri kushindwa wanakuwa tayari wamerudi nyuma na kushindwa kumalizia vitu walivyo vianza.

Lazima watu tutambue kwamba katika maisha kuna kufaulu na kufeli, na daima mafanikio yanakuja baada ya kufeli. Mfano kama umeamua kuanzisha biashara lakini ukaishia njiani kwa sababu ya kupata hasara. Lakini mara nyengine ukaamua kuanzisha biashara utakuwa tayari umepata uzoefu wa kutosha kuhakikisha kosa la kupoteza halijirudii tena.

Tambua kwamba mafanikio ni muendelezo wa kufeli. Na huwezi kufeli bila ya kuanza. Unatakiwa ufeli mara nyingi zaidi  ndio uweze kujifunza mafanikio. Na ipo njia moja tu ya kufeli moja kwa moja: Njia hiyo ni kushindwa kuanza.

Unapoamua kuanza ndio unakuwa umeanza kupiga hatua mbele. Hata kama umeanza kidogo lakini huo ndio mwanzo mzuri wa mafanikio . Usikubali kuendelea kuwa na hofu ya kuogopa kuanza.

Habari Njema Kwako.
Hofu kubwa ambayo inawarudisha watu nyuma ni kutokana na kuwa hawako tayari na kuanza. Tuchukulie mfano umeamua kuanzisha biashara ya kutengeneza pesa kwa njia ya mtandao kwa kutumia blogi. Unapoanza biashara hii utaona unahitaji kujuwa kila kitu kuhusiana na blogi. Hivyo utatumia muda wako bila ya kuupoteza kuweza kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na blogi. Wakati unaendelea kujifunza unakuwa na muda mzuri wa kujiandaa kutengeneza blogi ya kitaalamu. Kumbuka mwanzo unaanza ulikuwa unaona mambo ni magumu lakini unapokuwa kwenye mchezo kila kitu unakiona ni rahisi kwako. Na njia nzuri ya kujua kila kitu ni kuendelea kujifunza na kufanya kile ulichojifunza.

Hakuna siri nyengine ya mafanikio zaidi ya kuanza.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA