Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na tabia muhimu kwa kila
mfanyabiashara kuzifahamu kwa ajili ya kuwa na usimamizi mzuri wa pesa.
Usimamizi wa pesa ni ujuzi
muhimu kwa Mfanyabiashara yeyote anayetaka kufanikiwa katika maisha yake. Ni
muhimu pia kuzingatia matumizi mazuri ya pesa ili uweze kukua kimaisha.
Mafanikio katika biashara yako
yanategemea na ujuzi na ufuatiliaji wa tabia hizi za pesa kwa muda mrefu. Zijue
tabia hizi za pesa zinazomfanya kila mfanyabiashara aweze kujiletea mafanikio
makubwa katika biashara yake na maisha yake kwa ujumla.
Zifuatazo ni tabia za pesa
unazotakiwa kuzikuza ili kufanya vizuri katika biashara yako:
1.
Kupitisha Mawazo Ya Akiba
Kuokoa fedha ni muhimu sana kwa
maisha ya afya ya kifedha. Kuweka akiba kutakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya
pesa na hii utaweza kufanya matumizi yale ambayo ni ya lazima pekee. Utunzaji
wa pesa utakuwezesha kufanya matumizi ambayo umeyafanyia bajeti tu. Na hii ndio
inayowafanya wafanyabiashara kuweza kuwa na mtaji wa kutosha na kupelekea
ukuaji mzuri wa biashara anayoifanya.
Hatua muhimu ya kufuata ili
uweze kuweka akiba ni kujenga tabia ya kuhifadhi fedha kwanza kabla
hujafanya matumizi ya aina yoyote. Na hii unaweza kuifanya kwa kutenga kiasi
fulani cha pesa ambacho unaweza kukiweka kwenye akaunti maalumu ya biashara na
kufanya matumizi kutokana na mahitaji ya bajeti yako.
2.
Tumia Fedha Kwa Uangalifu
Kanuni muhimu ya kuwa
mfanyabiashara ni kwamba unakuwa mbahili katika pesa zako. Hakikisha pesa zako
hazitumiki kwa mambo ambayo hayaongezi faida kwenye biashara. Kutumia
pesa kwa uangalifu kutakusaidia kujijengea nidhamu mzuri ya pesa. Matumizi
mazuri ya pesa yatakusaidia kuokoa pesa nyingi na kupata mapato ya ziada.
Tabia hii ya kutumia kwa
uangalifu kutazalisha matokeo chanya juu ya biashara yako na maisha yako kwa
ujumla.
3.
Hesabu Kila Unachonunua
Kama mfanyabiashara ni wajibu
wako kufanya hesabu kwa kila shilingi unayoifanyia matumizi. Kufanya hesabu kwa
kila senti unayotumia kutafungua macho yako kwa matumizi yasiofaa. Hii
itakusaidia kuweza kuzuiya tabia mbaya ya matumizi mabaya ya pesa zako.
4.
Yape Kipaumbele Matumizi Yako
Ili kupata fedha yako moja kwa
moja, inakupasa kuanza kuendeleza tabia ya kuweka kipaumbele matumizi ya pesa
zako. Kutengeneza tabia hii itakusaidia kuamua ni bidhaa gani inahitajika kwa
wakati huo. Kuweka kipaumbele kwa mahitaji yako ya muhimu zaidi kunaweza
kukusaidia kuwa meneja mzuri wa pesa zako. Njia bora ya kila mfanyabiashara
mwenye mafanikio ni kuanza kutengeneza tabia nzuri ya kuwezesha ukuaji wa
biashara yako. Kupanga fedha yako ni mwanzo mzuri kwa ukuaji wa biashara yako.
Kama mfanyabiashara unayetafuta
mafanikio hakikisha unaendeleza tabia hizi. Hakiksha unaweka akiba, Unatumia
fedha kwa uangalifu, Unafanya hesabu kwa kila unachonunua na tumia kwa kuwa
kipaumbele.
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe
ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena