Jumatano, 23 Novemba 2016

Zijue Kanuni Tano (05) Muhimu Kwa Ajili Ya Kupata Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na kanuni muhimu kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako. 

Kila mtu anapenda afanikiwe. Mafanikio makubwa hayawezi kuja hivi hivi tu. Kama unataka kupata mafanikio makubwa, ni lazima ufanje zaidi ya kawaida yako. Ni lazima uchukue hatua kubwa zaidi. Lazima ndoto zako ziwe kubwa zaidi kuliko vile unavyotarajia.

Katika Makala hii nitakuelezea kanuni hizi tano ambazo zitakuweka kwenye njia sahihi itakayokupeleka kufikia mafanikio yako makubwa.

1.           Panga Malengo Yako Kwa Kiwango Cha Juu Unachoweza Kukifikia
Kwanza ni muhimu kuamini kwamba huwezi kufikia mafanikio makubwa pasipo na kuwa malengo uliyoyaweka wazi. Malengo yako ni ule uwezo wako wa kuona sasa hivi pale ambapo unataka kuwa katika maisha ya baadaye. Na hii ndio sababu muhimu ya wewe kuwa ni lazima uwe na ndoto kubwa. Panga malengo ambayo yatakusukuma wewe na kukutoa nje ya ukanda wa faraja yako ya kila siku. Lakini pia ni muhimu kuweka malengo ambayo unaweza kuyafikia ile usiweze kuchoka njiani na kupata msongo wa mawazo. Kama utakuwa umeelewa vizuri basi utakuwa tayari uko kwenye njia ya mafaniko.

2.           Chukua Hatua Ya Kufanya Mambo Makubwa
Kama huwezi kuruka basi kimbia. Kama huwezi kukimbia basi tembea. Kama huwezi kutembea basi tambaa. Lakini njia yoyote utakayopitia iwe ni kusonga mbele. Tambua kwamba haitoshi kupanga malengo pekee bali pia lazima uchukue maamuzi ya kufanya ili uweze kufanikiwa. Unapoweka malengo yako ni muhimu kuweka mfumo wa kukusaidia kuhakikisha kwamba malengo yako yote umeyapanga katika hatua na tarehe ya mwisho ya kuweza kuyafikia. Na kufanya hivyo hakikisha umeyavunja malengo yako katika hatua ndogo ndogo ambazo unaweza kufanya kila siku. Ukiweza kufanikisha mpango wa kwanza nenda kwenye mpango unaofuata. Jinsi unavyoweza kufanikisha malengo yako ndivyo zaidi unavyopata msukumo wa kufanya zaidi.

3.           Kubali, Ongea na Chukua Hatua Kwa Vitendo Kwa Yale Unayoyaamini
Ukitaka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni lazima ufunge mlango wa mawazo yako dhidi ya mambo yote yanayoweza kukukatisha tamaa. Kama utakuwa umefanya uchunguzi kwenye maisha yako ni kwamba utagundua siku zote kama unataka kufikia ndoto kubwa utaona kama akili yako inakwambia kwamba haiwezekani. Lakini ukweli ni kwamba kama unataka mafanikio makubwa ni lazima uende maili ya ziada isiyo ya kawaida. Lazima uiambie akili yako kwamba inawezekana. Zaidi unavyojenga Imani ndivyo hivyo unavyoweza kuondokana na hofu ya kushindwa. Wewe ndiye wa pekee unayeweza kujihamasisha kufikia mafanikio yako na tambua kwamba hawezi kutokea mwengine.

4.           Tenda Kwa Ujasiri Na Uadilifu
Uadilifu ni muhimu sana kama wewe ni mfanyakazi au mwajiri, mwanfunzi au mfanyabiashara. Uadilfu lazima uwe mzima usiogawanyika, uwe na uwezo wa kuzalisha matokeo sawa bila ya kujali mazingira gani uliyopo. Lazima ukuze maadili ya uaminifu na maadili yaliyo imara. Siku zote ukiwa muadilifu basi ujasiri hufuata.

5.           Fanya Ukaguzi Wa Kila Kitendo
Kila hatua lazima iwe na matokeo. Hivyo pima kitendo chako cha kabla na baada ya wewe kufanya ili kujua hasa athari ya tendo juu ya maisha yako na mafanikio. Jambo muhimu la kukumbuka katika vitendo vyako ni kwamba kila kitu kina umuhimu na kila kitendo lazima kilete matokeo.

Unapoweza kupanga mlengo yako kwa kiwango cha juu, unapochukua hatua ya kufanya mambo makubwa, Unapoweza kutenda kwa ujasiri na uaminifu na ukiweza kufanya ukaguzi wa kila tendo unalotaka kulifanya basi utakuwa umeweza kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA