Ijumaa, 25 Novemba 2016

Usiogope Kukosea Badala Yake Jifunze Kutokana Na Makosa Unayofanya


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana mafunzo unayoweza kuyapata kutokana na makosa unayoyafanya.

Ni kawaida kwa wanaadamu kufanya makosa kila siku, kuna makosa madogo na makosa makubwa ambayo tunayafanya. Makosa tunayoyafanya ni kama zawadi ambayo hutupatia muongozo wa kujifunza na kutufanya tukuwe kama watu.

Haya hapa ni mafunzo unayoweza kuyapata kutokana na makosa unayoyafanya.

1.           Makosa Yanatufunza Sisi na Yanaweza Kutupa Muongozo Jinsi Tunavyotaka Tuishi. Makosa yanatusaidia kuweza kujitoa. Makosa hutuongoza vile tunavyotaka tuishi. Makosa huweza kutuamsha na kutufanya tuwe makini kwenye mambo tunayoyafanya.

2.           Makosa Yanatufunza Tujikubali. Inawezekena kufurahia makosa yetu na baadaye kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuyafanyia masahihisho. Yaone makosa kama kituo cha kupumzikia kinachoweza kukupatia nguvu upya baada ya kuchoka.

3.           Makosa Yanatufundisha Namna Ya Kuondokana Na Woga. Kuna wakati unaweza kufanya juhudi zote lakini mambo yanakuwa magumu. Unapoweza kukabiliana na makosa mara nyingi hofu inaondoka.

4.           Makosa Yanatufundisha Jinsi Ya Kuongea Ukweli. Makosa yanatufundisha sisi tuweze kuongea ukweli. Unapofanya makosa na kuweza kukubali mbele za watu makosa uliyofanya inakujenga wewe katika kujifunza zaidi na kupelekea kukuwa.

5.           Makosa Yanatupatia Majibu Ya Kuweza Kujuwa Mambo Yanayoweza Kufanya Kazi Na Yale Ambayo Hayafanyi Kazi. Makosa ni kipimo cha kuweza kufanya uchunguzi. Unapoweza kupata uzoefu wa makosa yanayokutokea unapata ujumbe mzuri wa kugundua kipi kinweza kufanya kazi na kipi hakifanyi kazi.

6.           Makosa Yanatufundisha Kufanya Uadilifu. Mara nyingi makosa yanatutokea pale ambapo tumeshindwa kufuata utaratibu. Na makosa makubwa mara nyingi huanza na makosa madogo. Hivyo ni muhimu kuchunga uadilifu kwa mambo yetu tunayoyafanya siku zote. Makosa ni kama ishara ya maneno na vitendo vyetu kwamba haviendani sawa.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
hudhaifiali@gmail.com
       0784498867
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

Maoni 3 :

  1. Hongera kwa kazi nzuri
    Kweli "Tunajifunza" kutokana na makosa yetu Hakuna jipya kama hujakosa au hujawahi kukosea.

    JibuFuta
  2. Masomo yako yanavusha watu kuelekea mafanikio halisi

    JibuFuta

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA