Jumanne, 11 Oktoba 2016

Jifunze Njia Nane (08) Za Kuishi Maisha Kwa Kufuata Kanuni Zako


Kila mtu duniani ana utaratibu wake wa maisha. Ili kuweza kuishi maisha yako ya pekee usikubali kufuata watu wanavyotaka wewe uishi. Ni muhimu kujipangia utaratibu wako utakaoufuata na kukuwezesha kuishi vizuri.
Zifuatazo ni kanuni zitakazokuwezesha kuishi maisha yako:

1. Jifikirie wewe kama wewe

Kwa Nini Nafanya
 

Usikubali kila kitu unachoambiwa. Unapoambiwa kitu lazima uhoji na kufikria kwa umakini ndipo ufanye maamuzi. Unapofikiri kwa umakini kutakusaidia kupunguza kujuta na mawazo yasiyo ya lazima.

     
    2. Achana Na Mtazamo Wa Watu Wanavyokufikiria Wewe


Watu Wananionaje


Mtazamo wako ndio uko sahihi. Usijaribu kufuata kila kitu kutoka kwa watu. Fanya unayoyaamini . Yale unayoyaamini ndiyo yanayokufanya wewe uwe na mtazamo na maamuzi yako.
     
    3.  Usikate Tamaa



                 
Kushindwa Sio Mwisho Wa Maisha
 


Fahamu unachokitaka. Tengeza maisha yenye muelekeo ambao utafika kule unakotaka kufika.



4. Furahia Kazi Zako.

Furaha Ndio Kazi Yangu


Usikubali furaha yako iishie kwenye mikono ya watu wengine. Jipende mwenyewe na fanya kila kilicho kizuri kwa maisha yako. Jione kwamba wewe ni wa muhimu kuliko mtu yeyote kwenye maisha yako.
 
 
5. Jipe Moyo Wa Matumaini

Siogopi Changamoto na Najiamini


Jiamini. Chochote unachofanya fanya kwa kujiamini. Sema ukweli wakati wote ili uweze kujenga Imani ya kujiamini.
     
6. Shughulika na Kazi Zako


                                       
Haya Mambo Hayakuhusu


Usiwe mtu wa kushughulikia mambo yasiyokuhusu. Muda mwingi kuwa karibu na kazi zako na wala usifanye vitu ambavyo havina faida kwako.
     
7. Fanya Kazi kwa Vitendo



Ni Wakati Wa Mapambano
                                         

Usikae kimya,  uliza kila kitu. Tafuta taarifa, soma sana na fanyia kazi kila hatua unayojifunza.
     
8. Chagua Njia Yako



                       
Chagua Njia Yako
              


Hakikisha kila jambo unalolifanya unafanya kwa kujitofautisha na wengine. Fuata taratibu na kanuni zako ulizoweka. Fanya kitu ambacho hakuna mtu yeyote anaweza kukifanya.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA