Jumatatu, 10 Oktoba 2016

Hatua Kumi (10) Zitakazoifanya Blog Yako Iwe Ya Tofauti Na Kuweza Kukupatia Mafanikio Makubwa.


Watu wengi wanapenda kuanzisha blog kwa mtindo wa kuiga. Unapoanzisha blog kwa kuiga na kuchukua kazi za watu wengine ni kwamba blog yako haitoweza kufika  mbali. Ili Kuifanya blog yako iwe ya tofauti inawezekana ingawa inahitaji muda.
Ili kuifanya blog yako iwe ya tofauti na kuifanya iwe na mafanikio makubwa unahitaji kufuata hatua zifuatazo:
1.  Anzisha Blog. Kama bado hujaanzisha blog anza leo. Kuanzisha blog ni bure huhitaji gharama yoyote ile kwa kuanzia. Zipo baadhi ya blog ni za kulipia lakini pia zipo za bure. Unaweza kuchagua moja kati ya hizi. WordPress, Blogger, Tumblr, Medium, Weebly na nyengine nyingi.


2.  Chagua Mada ambayo unayoipenda. Hakikisha unachagua mada unayoipenda. Watu wengi wanapenda kusoma mambo yanayoweza kutatua changamoto zinazowakabili. Blog yako itakuwa ya tofauti sana ukiweza kuandika makala ambayo yataweza kutatua matatizo yao. Ukiweza kuandika makala  kwa kuweka na picha utaifanya blog yako ivutie zaidi. hivyo kuifanya blog yako kuwavutia wasomaji wengi.

3. Soma Sana. Unahitaji kusoma vitabu sana. Unahitaji kupitia blog za watu wengine ili kuweza kujifunza mbinu za kiuandishi na uzoefu wa watu wengine. Lazima  kila siku uwe mwanafunzi wa kuwa tayari kujifunza.

4. Fanya Ubunifu Kwenye Blog Yako. Hakikisha blog yako inakuwa ya kisasa kwa kufanya ubunifu wa templeti yenye kuvutia na yenye kushawishi wasomaji. Ifanye iwe rahisi na yenye kueleweka kwa kuzingatia ubunifu wa kitaalamu. Ifanye blog yako iwe ni rahisi kuonekana. Hii inawezakana kwa kutengeneza maneno ambayo yatakuwa na urahisi wa kuonekana. Ifanye mtu akitafuta basi iwe ni rahisi kuiona blog yako. Fanyia ubunifu kutokana na mahitaji ya msingi ya watu.

5Onesha muendelezo wa makala zako. Hakikisha unatuma taarifa kila siku. Unapotuma taarifa kila siku ni rahisi blog yako kutambulika na kupata watembeleaji wengi.  Vile vile kama blog yako itatoa vitu ambavyo watu wanavitafuta ni rahisi kwako kubaki kwenye ubora na kuendelea ukuaji wa blog yako.

6Bakia Kwenye Mada.  Kama unaandika kuhusu mafanikio basi baki kwenye makala za mafanikio. Kama hutoweza kubaki kwenye mada ni rahisi kuwapoteza wageni wanaotembelea blog yako.

7. Fanya Makala Za Kipekee. Hakikisha makala zako hazipatikani kwenye blog nyengine. Jaribu kubadili utaratibu watu waliouzoeya. Pangilia makala zako. Jinsi unavyoweza kupangilia kazi zako ndivyo hivyo hivyo blog yako itakavyoonekana kuwa na muonekano mzuri.

Hakikisha kila siku unatuma mambo yanayowashangaza watu.

8. Tangaza Blog yako. Ukiweza kufikisha makala kumi na tano( 15) anza kuitangaza blog yako. Zipo njia nyingi za kutangaza blog yako.

  • Weka taarifa zako kwenye mitandao ya kijamii.
  • Weka vichwa vya habari vionekane kwenye Google
  • Badilishana link ya makala zako na blog nyengine.

9. Kuwa karibu na wasomaji wako. Msomaji wa blog yako anapouliza maana yake ni kwamba anahitaji maelezo. Usidharau hakukisha unampatia majibu yenye kuridhisha.

10. Wajue wasomaji wako. Ni muhimu kujua wasomaji wako wanapenda nini. Hakikisha unafanya blog yako iwe na vitu ambavyo wasomaji wako watajifunza na kufaidika kwa uwepo wa blog yako.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA