Jumapili, 9 Oktoba 2016

Ruhusu Kuwa Wa Tofauti Iwe Ndiyo Kanuni Yako.


Watu wengi wanafikiri kuwa wa tofauti ni jambo lenye mtazamo hasi. Lakini hivyo sivyo ilivyo. Kuwa wa tofauti ni sehemu ya maisha.
Utofauti ninaouzungumzia hapa ni yale maamuzi ya kuwa mbishi. Au kwa lugha nyepesi ni kupinga au kwenda kinyume na watu wanavyotarajia. Wanaweza wakakuita mpinzani kwa yale mambo ambayo wamezoeya kuyafanya.

Hapa naweza kutoa mifano ya maamuzi ya msingi ambayo yanapelekea kuwa wa tofauti kwa wengine.
1.           Kuacha kazi yako ya kuajiriwa uliyoizoeya na kwenda kufanya biashara.
2.           Kuacha chuo na kwenda kuanzisha biashara.
3.           Kuondoka sehemu ya mji uliozaliwa na kwenda sehemu nyengine kutafuta maisha.
4.           Kufanya vitu kinyume kabisa na vile kila mtu anafanya.
5.           Kuazisha jambo ambalo halijawahi kufanywa.
Ni kawaida kwa watu wanaofanya vitu tofauti kuwasahihisha wale wafanyao makosa. Na wanapofanya hivyo ndivyo wanapotengeneza maadui, washindani na hata kuchukiwa na wengine. Mwisho kutamani bora kuondoka duniani.
Kuna methali isemayo “ Mwenye mafanikio ni yule ambaye hujenga msingi wake wa matofali lakini wengine wanakuja kuubomoa’’.
Tukirudi kwenye historia kuna watu mashuhuri duniani ambao walifanya vitu tofauti. Hawa walifanya mambo waliyoyaamini na kuyapigania mpaka mwisho.
Hakuna sehemu yoyote ya historia utakayosoma ukakuta kuna mtu ameibadilisha dunia au amechalenji mawazo ya taifa kwa kufuata mkumbo.
Hapa nakuwekea baadhi ya watu mashuhuri. Watu hawa  walifanya mambo makubwa katika hii dunia nadhani unaweza kuwatambua:

  • Muhammad
  • Sir Isaac Newton
  • Jesus Christ
  • Confucius
  • Saint Paul
  • Christopher Columbus
  • Albert Einstein
  • Galileo
  • John Locke
  • Henry Ford
  • Homer
  • Alexander the Great
  • Genghis Kahn
  • Thomas Edison
  • Sigmund Freud
  • Niccolo Machiavelli
  • Charlemagne
  • Adam Smith
  • Julius Cesar
  • George Washington

Wote hawa waliweza kufanya vitu kwa utofauti mkubwa na ndio maana mpaka leo tunawakumbuka na kuyafanyia kazi yale waliyoyafanya.
Hivyo naomba nikushauri na wewe pia uwe wa tofauti na hiyo ifanye iwe ndio kanuni yako ya maisha
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA