Jumamosi, 8 Oktoba 2016

Mabadiliko Huanza Na Chaguo.


Hakuna siku maalum kwa ajili ya kutafuta mabadiliko, tukiamua siku yoyote tunaweza kubadilika. Siku yoyote tunaweza kuamua kusoma kitabu ambacho kitakachoifanya akili yako kupata elimu mpya. Siku yoyote tukiamua tunaweza kuanza na mipango mipya. Tunaweza kufanya sasa hivi, au wiki ijayo au mwezi ujao, au mwaka ujao.

Vile vile tunaweza tusifanye kitu chochote. Tunaweza kuendelea kujidanganya kama tunafanya lakini hatuna tunachokifanya. Na kama mawazo ya kutaka mabadiliko yatatufanya tusiwe na amani, tunaweza kubaki kama tulivyo. Tunaweza kuchagua chochote lakini tukijipa sababu tutaishia na kuongea tu. Na kosa halitokuwa la dunia bali ni lako.
Uwezo tunao na wajibu tunao wa kufanya chaguo bora tutakaloweza kulianza leo. Yeyote anayetafuta maisha hahitaji majibu zaidi. Hahitaji muda zaidi wa kufikiri ili aweze kufikia maamuzi.
Hatuwezi kuruhusu makosa yatuhukumu, yajirudie kila siku na kutuongoza kwenye njia isiyo sahihi.  Lazima tuwe na misingi yote yatakayoleta utofauti mkubwa kwenye maisha.
Kutenda ni mhimili muhimu sana ambao haustahili kupuuzwa.
Wote wanaotafuta mafanikio na furaha tayari wametenda kazi nzito. Lakini pia hawakuweza kwenda kuchota tu hivi hivi. Tatizo ni kwamba ili tuweze kuwa na shauku ya matunda mema ni lazima tuweke akili, maarifa na nguvu kwenye vitendo vyetu. Kufanya bila ya kutumia akili na maarifa tunaweza kuharibu. Lakini tusipoteze muda mwingi kwa kutafuta akili.Vitu hivi huenda kwa makisio na uwiyano.
Ni rahisi kukosea wakati unapokuwa kwenye mwendo wa mafanikio. Na hii ndio maana kutenda kwetu tunatakiwa tuwe na mipango kazi. Lakini pia tuwe waangalifu sana ili tuweze kusonga mbele.
Vitendo vyetu lazima viwe na mipango. Lazima tutumie maarifa ya kutosha yatakayotuwezesha kupanga mipango leo kwa lile jambo unalotaka kulifanya kesho. Lazima tuwe na mipangilio ya baadaye, si tu kulala na kuota.
Kama tutakuwa na nidhamu kwenye mipango yetu, basi tutakuwa tunajitengenezea bahati mbeleni.
Safari yetu ya mafanikio sio kama Jumapili au Jumatatu unaamka na kuikuta siku. Hapana lazima tujipange na tuamue tunataka kuishia wapi. Lazima tuchague kituo na lazima tujiandae kupambana na changamoto zitakapotokea.
Kwa nini sisi wanaadamu ni viumbe wenye akili nyingi duniani. Lakini tunaziruhusu akili zetu kuishia katikati. Kwa nini tusiendelee ili tuweze kupata kile ambacho kinaendana na thamani yetu.
Sababu ni moja tu ya kwamba tumejipa uhuru wa kuchagua.
Katika hali nyingi chaguo linakuja kama zawadi. Lakini zawadi hiyo inapokuja katika hali ya kufanya kutokana na uwezo wetu, chaguo linabadilika badala ya kuwa neema linakuwa laana.
Mara nyingi tunachagua kufanya hafifu kuliko vile ambavyo tungeweza kufanya.
Kuna aina mbili za kuchagua:
Chaguo la kwanza ni kufanya ili upate kidogo kuliko uwezo wako. Kupata mshahara mdogo, kufikiri kidogo, kujaribu kidogo, kusoma kidogo, kuwa na nidhamu kidogo. Hili ni chaguo linalotupelekea tusiwe na mafanikio katika maisha.
Chaguo la pili ni kufanya kwa uwezo wetu wote kama tunavyostahili kuwa. Kusoma kitabu mwanzo mpaka mwisho. Kupata zaidi, kufanya zaidi, kutoa na kushirikiana kwa uwezo wetu wote.
Kwa nini tusichague kufanya kila kitu tunachoweza kufanya kwa uwezo na akili zetu zote.
Matokeo ndio kipimo sahihi cha maendeleo yetu. Sio mazungumzo wala maelezo marefu. Na kama matokeo yetu yamekuwa ya kiwango cha chini kuliko tunavyotarajia, maana yake ni kwamba tunatakiwa kuweka juhudi zaidi leo kuliko tulivyoweka jana.
Na zawadi kubwa na nzuri siku zote ipo kwa yule anayeleta thamani kubwa kwake na kwa dunia na kwa wote waliomzunguka. Na hii inatokana na uchaguzi wake.

Imeandikwa na Ali Khamis,
simu namba 0784498867.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA