Jumatano, 12 Oktoba 2016

Zijue Mbinu Sita Za Kuweza Kupata Mafanikio Kwenye Kazi Na Kwenye Maisha


Tunaishi ili tuweze kupata mafaniko. Mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi . Kazi tunazozifanya tunahitaji kuelewa mbinu zitakazotupa mafanikio makubwa.

Hizi hapa ni mbinu saba zitakazokusaidia kufikia mafanikio kwenye kazi zako na maisha yako yaweze kuwa bora:

1.           Jifunze:  Jipime kama unaweza kujifunza. Jifunze kila siku. Jifunze kile unachofanya kwenye kazi zako. Huwezi kufanikiwa kama hutojifunza. Kila siku mambo yanabadilka.

2.           Badili Tabia. Tabia zako ziendane na kile unachokifanya. Kazi zote huwa zina kanuni. Hivyo ni muhimu kufahamu kanuni zilizopo kwenye kazi zako. Na tabia njema siku zote ndiyo inayoleta mafaniko bora katika maisha. Kama umekubali kufanya kazi unayoifanya basi ni lazima ukubaliane na kanuni zake.

3.           Kuwa Na Tabia Endelevu. Tabia endelevu ndio kipimo pekee kilicho sahihi cha kupima mafanikio. Kama umeamua kujifunza hakikisha unajifunza kila siku. Kama umeamua kuamka  mapema hakikisha kila siku unaamka mapema. Kama una tabia njema hakikisha unaendeleza hiyo tabia. Unapojenga muendelezo wa tabia njema kutakusaidia kufikia maisha mazuri.

4.           Andika Hadithi Ya Maisha Yako. Fahamu Kwamba hakuna mtu mwengine atakayefanana na wewe.  Wewe ni wewe na hakuna mtu mwengine atakayekuja kufanana na wewe. Hakuna mtu anayeweza kutengeneza maisha yako. Kama umefanya makosa basi wewe ndiye wa kulaumiwa. Hakikisha unatengeneza hadithi ya maisha yako. Andika kile ambacho kipo kwenye akili yako. Ukishandika weka wazi dhamira yako kwa wengine. Baada ya hapo ishi na dhamira yako.

5.           Achana Na Mawazo Hasi. Mpango mzuri wa mafanikio ni kuachana na hadithi za kurudisha mafanikio yako nyuma. Achana na stori za kukatisha tamaa. Uwezo wa mafanikio unao utakapoamua kufanya.

6.           Fahamu Nguvu Mwendo. Fahamu kwamba binadamu tunasukumwa na nguvu mwendo. Ukiamua kukaa bila kufanya basi utaendelea kubaki hivyo hivyo hakuna mafanikio utakayoyapata. Ukiamua kufanya utaendelea kufanya mpaka pale itakapotokea nguvu nyengine itakayokusimamisha kufanya. Hivyo amua kuendelea kufanya usiruhusi nguvu ikusimamishe kwenye mwendo kasi wa kuendelea kufanya.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA