Tambua Kwamba Wewe Ni Wa Pekee Na Hakuna Mwengine Kama Wewe.
Tambua Wewe ni wapekee, umezaliwa kuwa wa tofauti na wengine. Hivyo ni lazima ueneshe vitu tofauti na wengine.
Kila mtu ana lengo la pekee ambalo haliwezi kuwa sawa na la mtu mwengine. Kila mtu ana kipaji chake maalumu na zawadi anayoweza kuwashirikisha wengine.
Tambua kwamba umezaliwa na vitu tofauti ambavyo hakuna mwengine mwenye navyo. Ukitaka kujua angalia alama za vidole kila mmoja ana alama tofauti.
Njia pekee ya kuweza kutambua zawadi tuliyonayo ni kufanya mambo yanayotufanya tuishi kwa furaha. Tambua furaha yako iko kwenye vitu gani. Tambua njia za kuishi kwa furaha na wafanye watu waishi kwa furaha. Unapopata muda wa kuwahudumia watu, huo ndio wakati wa kuonesha furaha yako kwa wengine.
Wewe ni mtu mwenye thamani sana na mwenye mvuto. Ilinde thamani hiyo na usiruhusu mtu achezee ubora wako. Fanya kila kilicho bora kwa nidhamu ya hali ya juu. Fanya kwa uadilifu na fanya kwa kujituma.
Kuwa na akili ya kuweza kujitofautisha na wengine. Onesha kipaji chako ili watu waweze kukutambua wewe kama wewe. Tafuta maarifa ya kutosha watu waweze kuona thamani yako. Usiruhusu akili za watu warudishe jitihada zako nyuma.
Thamini kila sehemu ya viungo vyako. Maamuzi yoyote utakayoyatoa kuhusu wewe yafanye kwa upendo mkubwa. Kubaliana na kila ulichonacho. Elewa kwamba wewe umekamilika, na wewe ni wa muhimu na una kila kitu cha kipekee.
Tukiweza kuzingatia na kujitambua kwamba kila mtu ni wa pekee, na kila mtu ni muhimu kutokana na anavyoonekana. Tunaweza kuifanya dunia iwe ni sehemu yenye kuwa na watu wenye kufanya vitu tofauti, lakini watakaoweza kuleta mafanikio makubwa.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena