Karibu tena ndugu msomaji wa
Makala hii. Leo nataka nikuelezee mambo yatakayokufanya uwe na maisha bora.
Mambo nitakayokueleza yatakufanya ubaki kwenye njia ambayo unaweza kuwa
na uwezo nayo na kupelekea maisha yako kuwa bora siku zote.
Kwenye kazi yoyote unayoifanya
kuna uzaifu na uimara. Hivyo ni vyema kufahamu uzaifu wako upo wapi na uimara
wako ulipo. Ukiweza kugundua wapi ndipo una nguvu zaidi hapo ndipo kwenye
maisha yako ya mafanikio. Kama bado umeshindwa kujua nguvu zako zilipo
hakikisha unajitoa katika kutafuta na uweze kukundua nguvu zako zilipo.
Ukiweza kujua wapi unaweza kuwa bora hakikisha unabaki hapo. Kama bado
unashindwa kujua nguvu zako zilipo wapi usiwe na wasiwasi endelea kufanya kazi
kwa bidii. Unapofanya kazi zaidi ndipo unapogundua uimara wako ulipo.
Mambo yafuatayo yatakusaidia
kuweza kufahamu uwezo wako na kipaji chako:
1.
Jiulize ni wapi unafanya vizuri.
Jiulize ni maeneo gani unaweza
kufanya vizuri. Ukijua ni wapi unaweza kufanya vizuri na kwa usahihi basi tumia
nguvu hizo ufanye kwa bidii hadi ufikie sehemu mzuri ya maisha yako.
2.
Kuwa Wazi.
Uwezo wako siku zote huwa uko
wazi. Jinsi ambavyo utakuwa muwazi na kufanya kwa umakini ndivyo hivyo
utakavyoweza kuona uwezo wako ulipo.
3.
Sikiliza Watu Wengine
Maeneo Wanayokusifia.
Sikiliza wengine wanasema nini
kuhusu wewe. Uwezo wako unaweza kuufahamu kupitia kwa watu wengine. Sikiliza
kwa umakini yale wanayoyasema na fuatilia. Unapofanya kazi kwa kiwango hafifu
hakuna ambaye atafurahishwa na kazi zako. Lakini unapofanya kazi kwa uwezo wako
watu watakusifia . Eneo ambalo umekuwa ukisifiwa endeleza na huo ndio uwezo
wako.
4.
Angalia Watu Waliokuzunguka.
Huhitaji kupoteza muda mwingi
kujilinganisha wewe na wengine. Unapojilinganisha wewe na watu waliokuzunguka
unatakiwa kujiuliza kwamba wao wanafanya kama wewe unavyofanya. Watu
waliokuzunguka wanafanya vizuri kuliko wewe. Unapojiuliza masuali ya kufanya
vizuri kuliko wengine itakusaidia kuweza kuwa wa tofauti na wengine. Tafuta
kitu kinachokufanya uwe tofauti na wengine. Endelezea hiyo tofauti yako mpaka
ufikie uwezo wako.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena