Watu wenye mafanikio makubwa
wanakuwa na hamasa ya mafanikio. Fahamu siri zao na zifanyie kazi ili na wewe
uweze kupata mafaniko.
Watu wenye hamasa za kipekee
wanalazimika kufanya zaidi kuliko kawaida. Watu hawa ni watu wenye heshima na
kuaminiwa na wengine. Ni watu wanaojiamini kwa kila kitu wanachofanya. Maisha
yao na ndoto zao zinakuwa hazina mipaka na wanaridhika na maisha yao.
Hawa ni watu ambao mtazamo wao
huwa ni ushindi daima, shauku ya mafanikio, na wanafanya mambo ambayo
huwafikisha kwenye safari yao ya mafanikio.
Hizi hapa ndio siri zao
zinazowahamasisha kuyafikia mafanikio ya kipekee:
1.
Wanakuwa na Hamasa ya Ndani.
Wanakuwa na nguvu ya ndani
inayowasukuma kuanza safari mpya, kuleta matokeo mazuri na kuweza kutatua
changamoto zao.
2.
Hawana Muda wa Kupoteza Kwenye
Malumbano.
Mara zote huwa wanaona mafanikio
na makosa ya wengine kama silaha ya kujifunza badala ya kuanzisha hoja za
kulumbana. Hawana muda wa kugombana wala kuanzisha mambo ambayo hayana
tija kwenye kuwaletea mafanikio.
3.
Wanakuwa na Nidhamu.
Wanapofanya makosa wanakuwa
tayari kukubali makosa yao na kuomba msamaha . Wanakuwa na moyo wa kuwapa
hamasa wengine na kushauri njia za kufanya zitakazowaletea mafanikio.
4.
Wanakuwa Wakweli.
Wanakuwa ni watu wenye mtazamo
wa kweli. Hawaishi kwa sababu ya kuwafurahisha wengine. Ni watu wenye kuwa na
misimamo ya kweli na wala hawayumbishwi na wengine.
5.
Wanakuwa na Mtazamo wa Mafanikio.
Watu hawa wana tabia ya kufanya
yale maeneo yenye kufanya kazi na yanayoweza kuwaletea mafanikio. Hawaangalii
historia mbaya bali wanaangalia mambo yaliyonyooka na yenye mtazamo wa
mafanikio.
6.
Wanafanya Zaidi Kuliko Kawaida.
Watu hawa wanaangalia mambo
magumu kuweza kupata kile wanachokitaka na wala hawachagui maeneo mepesi .
Wanafanya mambo ambayo hakuna mtu anayetegemea kuyafanya. Wanaamini uwezo wao
na wanakuwa na uhakika wa kufanikiwa.
7.
Wanaendelea Kujifunza.
Wanasoma sana na siku zote
wanatafuta taarifa mpya kwa umakini mkubwa. Ni watu wanaoelewa kwamba ili uweze
kukua ni lazima kujifunza.
8.
Wanafahamu Wanachotaka.
Mtazamo wao upo sahihi kuhusiana
na kile wanachokitaka kwenye maisha na wanakuwa tayari wanajua ni wapi wanata
kufika. Ni watu wasioruhusu kushindwa na mtazamo wao wanaamini kwamba kila kitu
kinawezekana.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena