Tatizo kubwa kwenye dunia
tunayoishi leo ni watu kukosa ufahamu wa maisha. Watu wengi wanaishi kwa
kufuata mkumbo. Tunaishi maisha ya kuiga na kuingia kwenye mtego wa kuishi
maisha yasiyo na muelekeo. Tumekuwa tukiishi kwa kutumia muda mwingi kwa
kufuata mazingira. Tufanya kile kinachotutokea ambacho hatujapanga kukifanya.
Tumesahau kubaki kwenye malengo na mipango yetu.
Kuwa na ufahamu na kuchukua
maamuzi kwa usahihi ya kuishi maisha yako ya kila siku kwa vitendo
kutakuwezesha kufikia malengo yako uliyojiwekea. Ishi kwa kuzingatia
madhumuni ya maisha yako. Fanya kutokana na thamani yako na usiwaruhusu
watu wakuamulie nini cha kufanya.
Unapoamua kufanya maamuzi ni
lazima kwanza kufikiri kama hayo unayoyafanya yanakupelekea kufika kwenye
malengo yako.
Kama kweli unahitaji kufikia
mafanikio ya uhakika. Ni muhimu kufuata funguo hizi tatu zitakazokufanya uishi
kwenye maisha ya mafanikio:
1.
Andika Malengo Yako.
Kitu cha kwanza unachokifanya
asubuhi unapoamka ndicho kitakacho onesha mwelekeo mzima wa siku yako. Andaa
mpango kwenye akili yako ambao utakupa nguvu mara unapoamka na amua kufanya.
Hakikisha unafanya hivyo kwa
kuyaandika malengo yako kila siku asubuhi. Baada ya kuandika weka alama kwenye
lile lengo muhimu kuliko yote. Lengo ambalo ni la muda mrefu ndilo litakalokuwa
na thamani kubwa kwenye maisha yako. Baada ya hapo jiulize “Ni hatua zipi
naweza kuchukuwa leo ambazo zitaweza kukuweka karibu na kuyafikia malengo
yako”. Andika hatua zote unazoweza kufikiria na zichague mbili ambazo ni
za muhimu zaidi. Ukishazichagua anza kwa kuzifanyia kazi kwa vitendo. Hakikisha
huachi kufanya mpaka zikamilike. Hii ni hatua muhimu sana ya kufanya mara
unapoamka. Kufanya hivyo kutaifanya kili yako iwe ni yenye kuzalisha.
Sababu nyengine ya kuyaandika
malengo yetu ni kwamba unapoyaandika inakufanya kila siku uweze kuyasoma. Na
ukiweza kufanya hivyo utajisikia vizuri sana. Mtindo wa kuyaandika ni ule wa
kama tayari umeshayafikia. Yasome na kuyarudia kila siku asubuhi ili uweze
kubaki kwenye malengo yako. Kumbuka malengo ambayo hayapo kwenye maandishi ni
vigumu kuyafikia.
2.
Tengeneza Mfumo Unaoweza
Kuuamini.
Jiamini wewe kwanza na amini
kile ambacho unakwenda kukifanya. Kama ukishindwa kijiamni hakuna atakaye
kuamini.
Kama kuna mtu atatokea kukuuliza
kuhusiana na malengo yako ya maisha, usiogope kusema. Hakikisha unasema kwa
sauti yenye kujiamini. Ikiwa leo hii atokee mtu akuulize kuhusu lengo lako la
maisha halafu utoe jibu la sijui basi wewe utakuwa ni mtu wa kushangaza sana.
Hatua muhimu ya kuishi na
kufanikiwa kwenye ndoto zako ni kuamini kile unachofanya. Ukiweza kuamini
kwenye akili yako kwamba tayari umefanikiwa malengo yako utakuwa umejenga hisia
za uhakika. Uhakika ambao utakusaidia kufanya kwa vitendo. Ukiweza kufanikiwa
kujenga mfumo wa uhakika utakuwa unakaribisha kuyapata mafanikio kwa urahisi
zaidi. Ukiweza kutengeneza mfumo wa twasira inayojirudia rudia kwenye akili
yako utakuwa umetengeneza nguvu ya kuyafikia mafanikio.
3.
Wekeza Wewe Mwenyewe.
Vitu ambavyo unaweza kuvifanya
kwa ajili ya uwekezaji huu ni kama vifuatavyo:
- Fanya
Mazoezi. Unapofanya mazoezi unaimarisha mwili wako uwe na
nguvu za kutosha kuweza kuzalisha zaidi.
- Kula
Vizuri. Kula chakula chenye afya kila siku kutausaidia
mwili wako uwe na afya njema.
- Anza
Kusoma Vitabu. Hakikisha unasoma vitabu vya kutosha. Unapoamua
kusoma hakiksha unaondoka na kitu cha kujifunza.
- Andika.
Usiruhusu kuondoka nyumbani bila ya kuwa na kalamu na karatasi. Wazo
lolote linalokuja kwenye akili yako hakikisha unaliandika muda huo huo.
Usiamini akili yako kama ndio itaweza kukumbuka kila kitu.
- Jifunze
Ujuzi Mpya. Kila siku hakikisha unajifunza kitu kipya. Kitu
kimoja kipya unachojifunza kwa siku moja ni sawa na vitu 365
utakavyojifunza kwa muda wa mwaka mzima.
Ushauri wangu wa mwisho ambao
naweza kukupa kwa leo ni kwamba hakikisha unaenda mbele. Rudia malengo yako na
fuata funguo hizi tatu za mafanikio ya maisha yako.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena