Jumatatu, 17 Oktoba 2016

Mambo Matano ( 05) Unayotakiwa Kuyaacha Kuyafanya Kama Unataka Mafanikio


Kila mtu anaweza kuleta tafsiri ya mafanikio kutokana na mtazamo na uelewa wake. Kwenye mafanikio yapo mambo ya msingi kwa kila mtu ambayo akiendelea kuyafanya yanaweza kuwa ndio sababu ya yeye kufanikiwa.  Vile vile kuna mambo ambayo mtu akiendelea kuyafanya yanaweza kuwa ndio sababu ya yeye  kutoweza kufanikiwa. Binaadamu tunao uwezo mkubwa wa kuzuiya mambo yanayokwamisha mafanikio yako.

Yafuatayo ndio mambo yanayo kwamisha mafanikio yako:

1.           Kutengeneza Visingizio
Kutenngeneza visingizio ni ile hali ya kila wakati hukosi sababu. Wewe unakuwa ni mtu wa kulaumu watu kwa sababu hujatimiza kile unacho kitaka. Acha kukataa majukumu yako pale unapofanya makosa. Kama umeshindwa hadi leo kufanikwa kwa sababu ya uchaguzi wako wa kimaskini, huna sababu ya kifikria mafanikio  uliyoyakosa kwamba yako nje ya uwezo wako. Naomba nikwambie kwamba watu wenye mafanikio hawafanyi hili kosa.  Usipoteze muda kwa kutengeneza visingizio kwa yale mambo ambayo umeshindwa kuyafikia. Visingizio havitokusaidia kufikia mafanikio.

2.           Mtazamo Hasi
Kama unataka kuvuna mafanikio ya maisha yako unahitaji kuangalia mambo mazuri.  Usitoe nafasi ya kufikria vitu hasi kwenye maisha yako. Muda wote kuwa na mtazamo chanya.  Mtazamo chanya hauwezi kuleta mafanikio ya maisha yako.

3.           Kuogopa Kufeli
Huna sababu ya kuogopa kufeli.  Kufeli kwako iwe ni msingi wa kujifunza na kuchukua hatua. Unapofanikiwa unaelewa kuwa umefanya vizuri. Unapofeli unaona kama umefanya vibaya na kujisikia vibaya. Ingawa kufeli kunaumiza lakini kama unataka mafanikio ni lazima uwe na mtazamo wa kufeli kama fursa ya kuelekea mafanikio.

4.           Kukata Tamaa
Unapokutana na vikwazo vya maisha usikate tamaa. Watu waliofanikiwa hawakati tamaa. Waliofanikiwa wanajitoa ili waweze kufika safari yao. Hawaruhusu vikwazo viwafanye wasiweze kujaribu tena.  Msingi mkuu wa mafanikio ni kujaribu kwa uwezo wako. Kama utaweka juhudi zako zote kwenye eneo unalolifanya bila ya kumuathiri mtu basi wewe utakuwa ni mtu uliyefanikiwa.
 
5.           Kuangalia Njia Nyepesi
Kwenye mafaniko hakuna njia ya mkato. Unatakiwa kujipa changamoto ya kufanya vitu vilivyoshindikana. Jivute hadi mwisho wa uwezo wako. Weka lengo la kufikia uwezo wako wa mwisho, na nenda zaidi ya hapo.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA