Ni ukweli usiopingika kwamba
tunaishi katika dunia iliyojaa kila kitu. Tumekuwa wa kupoteza muda mwingi
kufanya na kuangalia mambo yanayo tupotezea muda wetu. Kuachana na mambo yasiyo
na umuhimu katika maisha yetu sio tu yanaturahisishia maisha yetu lakini vile
vile tutaifanya akili yetu iwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya kufanya vitu
vyenye maana na kuishi maisha mazuri. Kuachana na mambo yasiyo na msingi
tunaipa akili uwezo wake wa kufikiri.
Haya hapa ndio mambo matatu ya
kujifunza yanayotoa nafasi ya kuishi maisha rahisi na yenye furaha kwa ajili ya
mafanikio yetu:
1.
Punguza Muda Wa Kuangalia
Luninga
Tunatumia muda mwingi wa kushughulika
na kuangalia vipindi kwenye luninga. Mara nyingi uzoefu unatuonesha ukiwa na
tabia ya kuangalia luninga unaweza kuishia kuupoteza muda mwingi hufanyi mambo
ya msingi na badala yake unatumia muda huo kuwa kwenye kioo cha luninga.
Kuangalia sana luninga kuna athari ya kutumia muda vibaya. Muda ambao ungeweza
kuutumia katika mambo ya uzalishaji na ukaweza kuleta mafanikio makubwa.
2.
Punguza Kuongea Maneno Matupu
Hii sina maana kwamba usiache
kuongea. Maana yangu ni kwama ni muhimu kuangalia maneno unayo yasema.
Maneno unayoyasema lazima yawe chanya. Maneno yawe yenye kuaminika na yenye
kuleta maana. Kusema maneno machache yenye ubora ni njia mzuri zaidi
kuliko kusema maneno mengi yasiyo na ubora.
3.
Punguza Muda Wa Kuangalia
Mitandao Ya Kijamii
Kutokana na nguvu ya
utandawazi katika ulimwengu wa sasa, mitandao ya kijamii imetufanya
kuzitawala akili zetu. Rahisisha maisha yako kwa kupunguza kuangalia
mitandao ya kijamii. Tumia muda mchache kwa kuangalia yale ambayo unaweza
kujifunza na achana kabisa na mambo ya kufurahisha yasiyokuwa na faida katika
maisha yako.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena