Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuwashirikisha
wasomaji wetu makala inayohusiana na Siri ya kuwa mjasiriamali mwenye
mafanikio.
Jee wewe una ndoto ya kuwa
mjasiriamali mwenye mafanikio? Kama bado una ndoto au tayari umeanza biashara
ni muhimu kufahamu jinsi ya kujenga biashara yenye mafanikio na kuelewa zaidi
mbinu bora za kiufundi kwenye biashara.
Madhumuni ya kweli na sababu ya
kutaka kuelekea kwenye safari yako ya mafanikio ni kufichua kipaji chako
kilichojificha. Kila mmoja wetu anacho kipaji ambacho ni muhimu kwa mafanikio
yake kama mjasiriamali. Katika safari ya ujasiriamali ni jambo la muhimu
kufichua na kukuza kipaji chako kilichojificha.
Kwa kweli kuwa na uwezo wa
kufanya mabadiliko na kuleta athari juu ya dunia lazima kwenda kupitia
mfululizo wa majaribio. Majaribio yako yanajiandaa kujenga msingi imara ambao
utakuwezesha kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio .
Kuweza kuwa mjasiriamali wa
kweli na mwenye mafanikio makubwa lazima ukubali kipaji chako na kiweze kupata
ridhaa ya familia na utamaduni wa jamii. Mara baada ya kipaji chako kutambulika
katika ngazi ya familia ndio utaanza kuchanua na kufanya makubwa juu ya dunia
hii.
Usiwe na hofu katika kuonesha
kipaji chako ambacho kinaweza kukusaidia kutengeneza mafanikio ya kuwa
mjasiriamali mwenye shauku kubwa ya kufanikiwa. Kimsingi, lengo lako liwe
katika kufichua na kukuza kipaji chako ili uweze kuwa na nguvu ya kuweza
kutimiza malengo yako.
Unapoweza kuonesha ujuzi wako wa
kiufundi na ukiweza kudhibiti hofu yako na kuweza kuondoa vikwazo
vinavyokukabili basi mafanikio ya kuweza kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio
hakuwezi kuepukika.
Weka email yako hapa na bonyeza
Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena