Jumanne, 29 Novemba 2016

Fahamu Mambo Magumu Matano (05) Kwa Kila Mfanyabiashara Mwenye Mafanikio Lazima Ayapitie

 
Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuendelea kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo magumu kwa kila mfanyabiashara mwenye mafanikio lazima ayapitie.

Watu wengi wanapaanza kuingia kwenye biashara wanajiona tayari wameyapatia maisha. Wanakuwa na ndoto kwamba ipo siku wataacha kazi wanazozifanya, na kufanya mambo wanayoyapenda na baadaye kuishi maisha ya kifahari.

Kuanzisha biashara ni mchakato mpana wa kuendelea kujifunza unaopelekea kubadili maisha yako. Ni mchakato ambao unaweza kukuongoza kwenye njia ambayo hukuweza kuitarajia na kuweza kufungua milango mipya ya mafanikio yako.

Kuanzisha biashara hadi isimame inahitaji juhudi sana. Inachukua muda wa kujitolea, nguvu na uwezo utakaokupeleka kwenye mafanikio. Ni lazima utakumbana na vikwazo na vikwazo hivyo haviangalii wewe ni nani.

Hivyo tambua kwamba unapokumbana moja ya mambo haya magumu jua kwamba hiyo ni kawaida kwa mfanyabiashara.

1.           Kuna Wakati Utahisi Kuchoka
Watu wanaposema kwamba kujifunza ujuzi wowote kunahitaji muda, wengi wetu tunataka mambo ya haraka. Matokeo yake watu wanapoteza muelekeo njiani na kuamua kufanya kitu chengine .

Kuanza na kubaki kwenye biashara ni sawa sawa na kumudu ujuzi mwengine . Biashara inahitaji uvumilivu na jukumu la kulea na kuikuza. Kuna wakati tunachoka na tunachofanya lakini kuna wakati tunaona mambo yanakuwa mazuri na tunayafurahia. Na hapa jambo zuri unalotakiwa kulifanya ni kubaki na kuendelea unachofanya bila ya kuchoka na kuacha kufanya.

2.           Biashara Inavyoendelea Kukuwa Ndivyo Utakavyokutana Na Changamoto Zaidi
Utapoanza biashara unakuwa na matumaini kwamba kila kitu kitaenda vizuri. Unakuwa na Imani kwamba hakuna kikwazo chochote kinachoweza kukutokea. Lakini hii ni njia ya kujipa matumaini mwanzoni unapoanza biashara. Ukweli ni kwamba biashara yoyote ile ina ugumu wake. Mara unapoanza hatua ya kujifunza jinsi biashara inavyokuwa hatua inayofuata lazima utakumbana na changamoto. Lazima usimame kwa miguu yako na jiandae kukabiliana na changamoto zinazokutokea. Fikiria hatua zitakazoifanya biashara yako kukuwa na fanya mabadiliko kutokana na mazingira yaliyopo.

3.           Wewe Huna Ujuzi Kama Unavyofikiria
Wengi wanapoanza biashara wanashindwa kujua uwezo wao. Wengi wanakuwa na mtazamo kwamba unajua kila kitu. Lakini ukweli ni kwamba huna maarifa ya kutosha kama unavyodhania.

Hiyo ni kawaida ni sehemu ya maisha . Jinsi unavyoweza kuwa na uzoefu kwenye hali zote mbili kufeli au kufanikiwa ndivyo unavyojenga ukomavu. Vile vile ni muhimu kujifunza kutoka kwa wale ambao wako mbele yako.

4.           Lazima Ujipe Kazi Tofauti Tofauti
Kazi nyingi zinahitaji kufanya kitu kinachofanana mara nyingi zaidi. Unapoanzisha biashara kwa upande mwengine maana yake ni kwamba unatakiwa kuelewa kila kitu. Ni lazima umudu maeneo yote ya biashara unayoifanya, na hii itakufundisha mambo mengi. Kuna wakati utajifunza kwenye kujaribu kitu kipya kuna wakati utajifunza kutokana na makosa unayofanya.

Nje ya biashara yako unaweza pia kujifunza kutokana na kusoma Makala na vitabu mbali mbali. Pia utajifunza katika kuhudhuria mafunzo au kuongea na watu wengine. Lakini kusoma ndio eneo ambalo unapaswa ulipe umuhimu wa pekee ili uweze kupata mafanikio unayoyataka kwenye biashara.

5.           Kuna Wakati Unaweza Kukata Tamaa
Nadhani umeshawahi kusikia watu wenye mafanikio wanaongelea kuhusu mambo magumu waliyopitia wakati wanaanza mpaka kufanikiwa kwao. Na wewe tambua kwamba utapitia njia hiyo hiyo. Kuna wakati unaweza kushangazwa kwa nini iko hivyo. Kuna watu watakukatisha tamaa kwa kile unachokifanya. Ikitokea hali hiyo wewe zidisha kufanya.

Tambua kwamba wafanyabiashara wote wametia kwenye hali ngumu kwa njia moja hadi nyengine mpaka kufika hapo walipo. Na kama wewe ni mmoja wao unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio ni lazima uungane nao kwenye mambo hayo magumu waliyoyapitia.

Jiunge Kupata Makala hizi
Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
hudhaifiali@gmail.com
  0784498867

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA