Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo muhimu ya kufanya kwa
ajili ya kukuletea hamasa ya mafanikio.
Hamasa ni chachu ya mafanikio.
Katika maisha ni muhimu kufahamu njia zitakazoweza kukupatia shauku ya
mafanikio, njia zinazoweza kukupa msisimko. Hakiksha unayajua mambo muhimu
yanayoweza kukukumbusha kila siku katika kukuwezesha kuwa na hamasa ya
mafanikio ya maisha yako.
1.
Fanya Kitu Ambacho Sio Cha
Kawaida Kwako.
Kwenye maisha ni lazima uamue
kufanya maamuzi ambayo yataweza kukufikisha kileleni. Nafikiri mpaka sasa
unapoendelea kunasoma Makala hii umeshafikiria ni jambo lipi kubwa unaweza
kulifanya kwenye maisha yako. Jambo hilo nina uhakika lipo kwenye akili yako.
Kama tayari hakikisha unalifanya kwa umakini wa hali ya juu na kuweka juhudi
zako zote.
Kumbuka maisha ni kama kivuli
ambacho kiko kwenye kiza. Mara unapoamua kwamba sasa nataka mabadiliko na
kwenda kwenye mwanga, na hapo ndipo maisha yako yatakapoanza kuwa tofauti na ya
kushangaza. Hivyo kila unalolifanya lifanye kwa kiwango cha umakini wa hali ya
juu.
2.
Tambua Vikwazo Vyako.
Ni muhimu kujua vitu ambavyo ni
vikwazo kwako. Tambua mambo ambayo yanaweza kukurudisha nyuma. Gundua mambo
ambayo yatakupelekea wewe ukwame. Ukiweza kujua vitu ambavyo vitakupelekea wewe
ukwame itakurahisishia kuona njia ya kutatua mambo yanayoweza kukukwamisha.
3.
Kuwa Na Watu Sahihi.
Hakikisha watu wako wa karibu
wanakuwa na mtazamo chanya dhidi yako. Ni muhimu watu wako wawe na malengo
mazuri kwenye maisha yao. Zingatia kuchagua marafiki ambao wana mtazamo wa
mbali kwenye maisha wanayoishi. Epuka kuwa na marafiki wenye mtazamo hasi.
Achana na watu sumu wenye kulaumu kwa kila jambo.
4.
Yajali Maisha Yako.
Chukua tahadhari kubwa kuhusiana
na afya yako. Kula vizuri na fanya mazoezi. Hakikisha unakula chakula kizuri
kwa ajili ya kuimarisha afya yako. Fanya kazi endelevu na kuwa na muda wa
mapumziko. Hakiksha unalala mapema na kuamka mapema.
5.
Jione Wewe Kuwa Ndiye Bora.
Katika eneo lolote ulilochagua
kwenye maisha yako hakikisha unafanya kwa kiwango cha juu. Na jambo lolote
unalolifanya elewa kwamba linaanzia na mawazo yako.
6.
Endelea Kusonga Mbele.
Hakikisha chochote unachofanya
kwenye maisha yako kinaendelea. Fanya kwa mwendo wa haraka kuhakikisha kwamba
unafanya na wala hakuna kitu kitakachokufanya wewe usimame. Jinsi unavyoweza
kufanya kwa haraka zaidi ndivyo hivyo unavyojenga misingi ya mafanikio. Kama
umepanga kufanya jambo kwa mwaka mmoja hakikisha unalikamilisha ndani ya
kipindi cha miezi sita.
Hivyo kama unataka mafanikio ya
maisha yako hakikisha unafuta mambo haya sita yatakayoweza kujenga hamasa
kwenye mafanikio yako.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena