Ijumaa, 9 Desemba 2016

Panda Mbegu Bora Uvune Maisha Yenye Mafanikio



Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na upandaji wa mbegu bora kwa ajili ya maisha yako ya mafanikio.

Kuna Msemo wa Kiswahili unasema upandacho ndicho uvunacho. Msemo huu una maana mzuri na ni muhimu kuufahamu. Mkulima siku zote anapopanda mahindi anategemea avune mahindi,  Huwezi kupanda mahindi na ukavuna nyanya.

Mbegu  bora ambayo utaipanda leo kwenye maisha yako ni msingi mzuri kwa maisha yako ya baadaye. Sasa ni uamuzi wako wa kuamua kupanda leo kile ambacho utavuna kesho.  Kitu ambacho kipo karibu  yako ni kupanda kwenye udongo bora wenye rutuba. Baada ya hapo hakikisha mbegu yako inapata virutubisho vya kutosha. Mbegu yako inahitaji upendo, mbegu uliyoipanda inahitaji muda, inahitaji kuvumilia na inahitaji uwezweshaji wa kutosha ili iweze kufanya vizuri.

Kumbuka kwamba mbegu ndogo inaweza kuleta mazao mengi.  Kama ni mtoto basi anaweza kuwa bingwa kwenye hii dunia. Mbegu mia za papai unaweza kutoa mapapai zaidi ya elfu moja. Unapoweza kuongeza ukubwa wa unachofanya ndivyo hivyo hivyo unavyoweza kuongeza mafanikio ya maisha yako. 

Hakuna ambaye anayeweza kutengeneza mafanikio yako , na hakuna mtu ambaye anaweza kuongoza maisha yako pasipo kuwa na ridhaa yako ya kutaka. Na hakuna ambaye anao uwezo wa kukusimamisha wewe usifanikiwe.  Juhudi zako na maarifa ziweke kwenye eneo ambalo litakuletea mafanikio. Usifanye kitu ambacho hakitaweza kuleta mafanikio yako. Jiandae kupanda mbegu ya mafanikio mara elfu moja zaidi.

Siri ya mafanikio yako imefichwa na kile unachokifanya kila siku. Jinsi unavyoweza kutatua matatizo  ya wengine ndivyo unavyokaribisha mafanikio yako.


Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA