Habari za leo ndugu
msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa
makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na umuhimu wa Kujiwekea
Malengo Makubwa.
Watu wengi katika dunia
ya sasa tunaishi bila ya kuweka malengo. Watu wengi tunaishi kwa sababu tu tupo
tumezaliwa tunatakiwa kuishi. Tukifanya tathmini ya watu ambao wanajiwekea
malengo kwenye maisha yao ni ukweli usiopingika kwa hawatazidi asilimia kumi.
Sababu kubwa ya watu kutoweka malengo ni kuwa hawana uhakika wa kile
wanachokifanya. Hajui anafanya nini sasa, atafanya nini kesho na anataka
kufanya nini kwa muda wa mwaka mzima.
Ndugu yangu kuweka
malengo inakupa muda wa kujitathimini kwenye maisha yako kwa ujumla. Kuweka
malengo inakusaidia kujua kama unaenda mbele kwenye maisha yako ama unarudi
nyuma.
Kwa nini unahitaji
kuweka malengo makubwa kwenye maisha yako?
Zipo sababu nyingi ni
kwa nini unahitaji kuweka malengo makubwa lakini kwa leo nitakupa sababu hizi
tano(05):
1.
Fahamu kwamba uwezo unao
mkubwa. Uwezo unao mkubwa lakini mpaka
sasa hujaweza kuutumia. Kama uwezo wako ulionao unaendelea kuutumia katika
kufanikisha malengo ya watu wengine ni bora kuanzia leo ukafikiria njia tofauti
na hiyo. Maana nikuambie rafiki yangu kama unaishi kwa kufanikisha malengo ya
watu wengine basi akili yako unaidumaza. Eti unajipa sababu ya kwamba mimi
nimesoma ili niajiriwe. Tabia hiyo inakujenga usiweze kufikiria njia nyengine
inayofaa na uwezo wako mkubwa ulionao. Jiandae kutoka huko ili uweze kuutumia
uwezo wako mkubwa ulionao.
2.
Fahamu Kwamba Unastahili
Kuishi Maisha Bora. Hukuzaliwa kufanya kazi ambayo huipendi,
hukuzaliwa kutumia muda wako wote kwenye utumwa. Umezaliwa kuwa na maisha bora
na ya kipekee. Tumia uwezo wako na kipaji chako na fanya kitu ambacho
unakipenda kwa ajili ya kuishi maisha bora. Huwezi kuwa na maisha bora kama
utashindwa kufanya kitu ambacho unakipenda.
3.
Fahamu Muda Na Pesa Ndio
Rasilimali Muhimu Kwako. Wezi ni wengi, usumbufu
ni mwingi na kila mtu anawinda rasilimili zako. Usikubali kila mtu awinde
hela zako na muda wako. Hizo ndio rasililimali zako ambazo zinakuwezesha
kupanga mambo makubwa yanayotoa uzalishaji bora na maisha yatakayokuletea
mapinduzi makubwa.
4.
Weka Malengo Yasiyo Ya
Kawaida. Fahamu wewe ni wa pekee, Huna sifa ya
kufanya kile ambacho kila mtu anakifanya. Unatakiwa uwe tofauti na mkumbo
wa watu. Weka dhamira ya kweli ambayo yataweza kukutofautisha wewe na wengine
na kukufanya kuwa mbali na kawaida. Usifanya kwa sababu eti jana nimefanya bali
fanya kwa sababu umeamua kufanya kutokana na malengo uliyojiwekea ambayo siyo
ya kawaida.
5.
Fahamu Kwamba Unahitaji
Kwenda Mbele Na Sio Kurudi Nyuma. Jipe uhakika kwamba
hakuna kitu ambacho kinaweza kukuzuia kusimama kuanzia sasa. Anza hapo
ulipo sasa na usisisubiri mpaka ukamilishe mtaji. Muda sio rafiki sana na saa
zinaenda kwa kasi ya ajabu.
Hayo ndio mambo matano
ambayo nimekuandalia kwa leo msomaji wangu na mfuatiliaji wangu mzuri wa Makala
zangu. Nakuahidi sitokuangusha nitakuletea kile kilicho bora kwa
mafanikio ya maisha yako. Hivyo endelea kunifuatilia na kusoma Makala zangu
zenye kuleta hamasa na ubora wenye mafanikio. Sitokubali kamwe kukuacha hivi
hivi. Tutakuwa wote hadi kilele cha mafanikio.
Weka email yako hapa na
bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email
yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena