Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na makosa manne tunayotakiwa kuyaepuka ili tuweze kufikia malengo yetu katika maisha.
Haijalishi umejiwekea malengo kiasi gani , ndoto zako ni zipi au mabadiliko yoyote yale unayotaka kuyafikia kwenye maisha yako, lakini ukweli kwako na kwa watu wengine ni lazima ujitoe, ufanye kazi kwa bidi na uwe na maono ya kutia hamasa ya kufikia mafanikio. Hakuna njia ya mkato ambayo unaweza kuipata ya kubadili maisha yako au kufikia malengo yako na ndoto ambazo unaziota bila kuwa na vitu hivi vya msingi.
Unaweza ukawa unalitambua hili, lakini linapokuja jambo la kufikia malengo wengi wetu huwa tunaanza vizuri lakini baaaye tunasima, baadaye tena tunaanza upya halafu tunasimama tena na mwisho wa siku tunakata tamaa kwa sababu ya mambo kuwa magumu.
Nakumbuka 2015 nilijiwekea malengo Matatu makubwa ambayo nilitarajia kufikia 2016 niwe nimeyatekeleza. Lakini mpaka sasa nimekamilisha nusu tu ya lengo moja kati ya hayo matatu. Haya mengine hata robo sijayafikia. Na mwaka 2016 ndio umeisha na sijakamilisha hata lengo moja.
Nimetafari kwa kina na kujiuliza ni kwa nini naendelea kugonga kwenye ukuta pasipo na kufika malengo yangu.
Nimegundua sababu kubwa ni kwamba tunashindwa kuyaepuka makosa haya ambayo yanatupelekea tushindwe kufikia malengo tuliyojiwekea.
1. Tunatarajia Matokeo Ya Haraka
Kosa hili linaweza kuwa na athari kubwa kwenye Imani yako na mtazamo wa kufanikiwa. Kama unataraji kupata matunda ya haraka na ukashindwa kuyapata, maana yake kitakacho kutokea ni kwamba utapoteza Imani ya malengo ambayo ungeweza kuyafikia. Usijaribu kupuuzia uwezo wa subira linapokuja suala la kuweka na kufanya kazi kuelekea malengo na ndoto zako.
Ni uvumilivu wako utakaofanya kufika kwenye safari yako ya mafanikio.
2. Kuwa Na Mtazamo Wa Kushindwa Kama Sababu Ya Kukata Tamaa
Kwenye maisha unapoweza kukabiliana na changamoto za kushindwa ndio unavyokuwa na udhibiti mzuri wa maisha yako. Wewe ndiye unayeweza kuchagua ni kwa namna gani njia ya kushindwa unataka iathiri maisha yako. Unaweza kuchagua kukata tamaa ama kusimama na kuendelea mbele.
Unapokuwa na changamoto ya kushindwa ichukuwe kama sehemu ya kujifunza na muongozo wa pale ulipokosea.
3. Kushindwa kwa Kutarajia Au Kupangia Yasiyotarajiwa
Maisha bila malengo tarajia usichokitarajia kinaweza kukutokea. Mara nyingi kama hujajiandaa kwa jambo ambalo hujalitarajia kutokea likitokea huwa linaleta madhara makubwa.
Njia bora ya kuweza kuyadhibiti usiyoyatarajia ni kujiandaa kupanga yale usiyoyatarajia.
Na hatua muhimu za kupanga kwa yale usiyoyatarajia ni.
- Ufahamu wa yale usiyoyatarajia
- Jiandae na usiyoyatarajia kwa kuweka mpango kazi.
- Jitoe kwa kusonga mbele malengo na ndoto zako.
4. Kuchoshwa Na Mambo Unayotakiwa Kufanya Kila Siku
Ili kuweza kufanikiwa kupata unachokitaka ni lazima ubadilike. Fanya vitu tofauti, Jenga tabia tofauti na kuwa na mawazo tofauti. Vyote hivyo havitokei kwa usiku mmoja. Bali vinatokea kwa kurudia kufanya matendo yako kila siku.
Kuwa tayari na matokeo ya kuchoshwa na yale unayoenelea kufanya kila siku. Lakini hiyo fahamu kwamba hiyo ndiyo njia sahihi ya kuweza kuyafikia mafanikio ya malengo na ndoto zako.
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena