Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuwashirikisha
wasomaji wetu makala inayohusiana mafunzo unayoweza kuyapata kutokana na makosa
unayoyafanya.
Ni kawaida kwa wanaadamu kufanya
makosa kila siku, kuna makosa madogo na makosa makubwa ambayo tunayafanya.
Makosa tunayoyafanya ni kama zawadi ambayo hutupatia muongozo wa kujifunza na
kutufanya tukuwe kama watu.
Haya hapa ni mafunzo unayoweza
kuyapata kutokana na makosa unayoyafanya.
1.
Makosa Yanatufunza Sisi na
Yanaweza Kutupa Muongozo Jinsi Tunavyotaka Tuishi. Makosa
yanatusaidia kuweza kujitoa. Makosa hutuongoza vile tunavyotaka tuishi. Makosa
huweza kutuamsha na kutufanya tuwe makini kwenye mambo tunayoyafanya.
2.
Makosa Yanatufunza Tujikubali.
Inawezekena kufurahia makosa yetu na baadaye kufanya kazi kwa bidii ili kuweza
kuyafanyia masahihisho. Yaone makosa kama kituo cha kupumzikia kinachoweza
kukupatia nguvu upya baada ya kuchoka.
3.
Makosa Yanatufundisha Namna Ya
Kuondokana Na Woga. Kuna wakati unaweza kufanya juhudi zote
lakini mambo yanakuwa magumu. Unapoweza kukabiliana na makosa mara nyingi hofu
inaondoka.
4.
Makosa Yanatufundisha Jinsi Ya
Kuongea Ukweli. Makosa yanatufundisha sisi tuweze
kuongea ukweli. Unapofanya makosa na kuweza kukubali mbele za watu makosa
uliyofanya inakujenga wewe katika kujifunza zaidi na kupelekea kukuwa.
5.
Makosa Yanatupatia Majibu Ya
Kuweza Kujuwa Mambo Yanayoweza Kufanya Kazi Na Yale Ambayo Hayafanyi Kazi. Makosa ni
kipimo cha kuweza kufanya uchunguzi. Unapoweza kupata uzoefu wa makosa
yanayokutokea unapata ujumbe mzuri wa kugundua kipi kinweza kufanya kazi na
kipi hakifanyi kazi.
6.
Makosa Yanatufundisha Kufanya
Uadilifu. Mara nyingi makosa yanatutokea pale
ambapo tumeshindwa kufuata utaratibu. Na makosa makubwa mara nyingi huanza na
makosa madogo. Hivyo ni muhimu kuchunga uadilifu kwa mambo yetu tunayoyafanya
siku zote. Makosa ni kama ishara ya maneno na vitendo vyetu kwamba haviendani
sawa.
Weka email yako hapa na bonyeza
SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
hudhaifiali@gmail.com
0784498867
Hongera kwa kazi nzuri
JibuFutaKweli "Tunajifunza" kutokana na makosa yetu Hakuna jipya kama hujakosa au hujawahi kukosea.
Asante sana
FutaMasomo yako yanavusha watu kuelekea mafanikio halisi
JibuFuta