Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na kufanya chochote unachotaka
kufanya kwenye maisha yako kinawezekana.
Unaweza kufanya chochote kwenye
maisha yako. Na ukiamua kufanya hakuna unachoweza kushindwa. Tambua kwamba
hakuna muda wa kusubiri ili uweze kuanza. Msingi wa yote hayo ni kujipangia
malengo na mipango ili uweze kufanikiwa. Na mbinu sahihi ya kufanya chochote
unachotaka kukifanya ili uweze kujiletea mafanikio ni kupenda kile unachotaka
kukifanya na kifanye kwa furaha. Pia usiruhusu kitu chengine kiondoe furaha
yako.
Hizi hapa ni njia sita (06) zitakazoweza
kukufikisha kwenye safari yako ya mafanikio:
1.
Jifunze Kitu Kipya
Jinsi unavyoweza kujifunza zaidi
ndivyo ambavyo unavyoweza kuongeza maarifa. Unaweza kuona vitu unavyovipenda ni
vile vinavyokupatia furaha. Na vitu hivyo ndivyo vinavyoweza kukupatia furaha
kwenye maisha yako.
Upo uzoefu ambao hauna mwisho.
Fanya mambo mengi tofauti na usipende kujiwekea mipaka.
2.
Andika Ndoto Zako Zote
Andika kila kitu ambacho kipo
kwenye ndoto zako na kile unachotaka kukifanya kwenye maisha yako. Hakikisha
unachoamua kufanya kinakuletea furaha. Ukimaliza kuandaa orodha yako pangilia
upya kile ambacho ni muhimu zaidi na kitu hicho kiwe cha mwanzo kukifanya.
Usiogope kuwa na ndoto ambazo
zitakuchukua muda mwingi kuweza kuzikamilisha. Muda ni jambo dogo sana kama
utaamua kufanya kitu ambacho unakipenda.
3.
Tengeneza Dira ya Maisha yako
Dira yako itajengwa kutokana na
mawazo yako uliyonayo. Na hii ndiyo inayobeba sura mzima ya maisha yako, ndoto
zako na mwelekeo wa kile unachotaka kufanya kwenye maisha yako.
4.
Tambua ni Kitu Gani Kinahitajika
Ili Uweze Kufika
Ili uweze kufanya kitu chochote
unachotaka ni muhimu kujuwa vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kuweza
kukufikisha huko. Kama ni mafunzo yanahitajika basi hakikisha unapata mafunzo
ya kutosha. Kama ni pesa zinahitajika basi usiogope kutumia pesa ili ziweze
kukupatia thamani unayoitafuta.
5.
Tengeneza Mpango Kazi Wa Miaka
Mitano
Usifikirie kitu pekee cha
kukufikisha pale unapotaka kwenda , lakini pia fikiria kuandaa mpango kazi wa
miaka mitano na jinsi unavyoweza kufika. Tengeneza mchanganuo ambao
utakuwa na vitu vyote vya msingi. Na hiyo itakuwa ndiyo njia yako
itakayokuongoza.
6.
Fanya Hatua Kwa Hatua
Kama malengo yako unayotaka
kuyafanya ni makubwa ambayo yatachukuwa muda mrefu, yagawanye sehemu ndogo
ndodo ili yaweze kuwa rahisi kuyatekeleza. Na njia hii itakusaidia kukutia
hamasa ya kufanya zaidi na kupelekea kufikia mipango yako.
Hakikisha unajua nini unachotaka
kufanya na ni muhimu kuandaa mpango kazi ambao utakufikisha na kupata chochote
unachotaka kufanya. Usikate tamaa kwenye dunia hii ukiamua kufanya hakuna
kinachoweza kukushinda.
Weka email yako hapa na bonyeza
SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena