Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na njia tano unazotakiwa
kiziishi ili uweze kukumbukwa kwenye maisha yako.
Kuanzia sasa ni lazima tutambue
kwamba tunazo nguvu za kuacha athari chanya kwenye maisha tunayoyaishi katika
dunia. Ni lazima kujitoa katika kila nafasi unayoweza kuipata. Ni muhimu
kuyafanya maishi yako yawe zawadi. Siku ukitoweka duniani watu wanatakiwa
waendelee kukukumbuka wewe kwa yale mazuri uliyoyafanya duniani.
Yapo makundi matano ambayo
unaweza kuyafanya ili watu waendelee kukukumbuka kwa mazuri uliyofanya:
1.
Kijamii: Yaguse Maisha Ya
Wengine
Japokuwa kila mtu anakuwa na
ndoto zake na matumaini katika maisha. Lakini watu wengi wanakuwa wapo tayari
kusubiri na kupokea mabadiliko na ushauri wa maisha kutoka kwa wengine. Kuwa
sehemu ya mchango mkubwa kwenye jamii kwa kutoa huduma ambayo itaweza kuwafikia
watu wengi zaidi.
2.
Binafsi: Jiangalie Wewe Mwenyewe
Wewe ni wa pekee. Hakuna mtu
ambaye atakuja kufanana na wewe. Fanya kitu ambacho ukikifanya kinaweza
kuwafikia wengine. Na kitu kizuri ambacho unaweza kukifanya na kuendelea
ni kuandika. Unaweza kutengeneza blog na kuanza kuandika makala ambazo
zitawafikia watu wengi au unaweza kuwa unaandika vitabu. Njia hii ya kuandika
mara nyingi inawafikia watu wengi kuweza kupata maarifa ambayo yanaweza kudumu
kwa muda mrefu.
3.
Kimwili: Mwili wako ndio mali
kwako
Miili yetu ni thamani muhimu
kwetu. Tumezaliwa tuweze kutumia maarifa yetu yote. Hakuna mtu wala jambo la
kulaumu katika maisha yetu. Miili yetu ina nguvu za kutosha kuweza
kufanya kitu chochote. Tumia nguvu ulizonazo kwenye mwili wako katika kufanya
mambo yaliyo bora yanayoweza kukufanya wewe uonekana shujaa wa maisha yako.
4.
Kiroho: Angalia Imani Yako
Jenga hisia ya kuiona dunia kama
ina maana sana kwako. Sote tuna kitu ambacho huzifanya roho zetu zipate Amani
na furaha. Fanya unachofanya kwa uaminifu na kwa moyo wa upendo.
Unapofanya kwa roho ya upendo na uaminifu unakuwa umetengeneza heshima ya
kutambuliwa na kukumbukwa daima.
5.
Akili: Akili yako ndio kitovi
cha udhibiti
Akili zetu ndizo zinazotuongoza
nini tufanye. Mawazo yako yaweke katika kuwasaidia watu wengine kupata kile
wanachokihitaji kwenye maisha yao. Thamini watu wote na ishi kwa kuwa na msaada
kwa maisha ya watu wengine. Jitoe katika kuwafanya wengine wawe na maisha bora.
Hizi ndio njia tano bora za
kuishi maisha yako ili watu waweze kukukumbuka. Chagua kuishi kwa kufuata njia
hizi kwa ajili ya kuacha athari kwenye dunia hii.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena