Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mbinu za kuendeleza mawazo
ya mafanikio.
Kama ungependa kuwa na mafanikio
Zaidi katika maisha yako, fanyia kazi mawazo yako ili uweze kupata muongozo wa
mafanikio.
Na hizi hapa ndio mbinu
ninazokushauru uziendeleze kwa ajili ya mafanikio yako.
1.
Jifunze Kutafakari kwa Mtazamo Mpana
Ondoa Dhana ya kwamba
haiwezekani kwenye jambo lolote unalofanya. Unapoweza kufikiria mambo makubwa
na kuamini kwamba inawezekana, hapo ndipo akili yako inapoweza kuwa na mtazamo
wa kuweza kufanya bila kushindwa. Kila kitu kinawezekana, ni juu yako wewe dhidi
ya kufanya kwa upendo na kwa bidii ili kuweza kufikia maisha ya mafanikio. Waza
mambo makubwa ambayo yatakupeleka hatua kumi mbele kufika kwenye maisha ya
mafanikio. Na unapoamua kufanya usikate tamaa.
2.
Fanya Maamuzi Sasa kwa Ajili Ya
Kuweza Kuishi Maisha Mazuri Baadaye
Fikiria maisha yako ya usoni.
Huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako bila ya kuwa na mtazamo wa baadaye. Lazima
uishi kwa kufanya mambo ya msingi sasa ili uweze kuishi vizuri baadaye. Lazima
ufikirie ni maisha ya aina gani unataka kuishi.
Mtazamo wa baadaye unaweza
kukuongoza katika kufanya maamuzi yako ya kuishi maisha ya kila siku.
3.
Chukua Hatua Kwenye Wakati Mgumu
Moja ya njia mzuri ya kujenga
kujiamini ni kuchukua hatua kwenye hali isiyo ya kawaida. Unapoweza kujifunza
kufanya kwenye wakati mgumu unakuwa umetengeneza uwezo wako wa kuwa jasiri na
kuwa na kasi ya kujenga. Chukua hatua moja kila siku ya kufanya jambo ambalo
hujatarajia kulifanya. Jifunze kufanya kitu hata kama unaogopa kufanya. Fanyia
kazi malengo makubwa na jenga maisha yako kwa ndoto ambazo zitakutoa kwenye
hali ya kawaida.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena