Jumanne, 15 Novemba 2016

Jifunze Njia Tatu (03) Za Kufikiria Kama Milionia


  Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

 Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo matatu ya kujifunza ili uweze kufikiria kama milionia.

Watu wengi wanadhani kwamba kuwa milionia ni suala la kuja na wazo la biashara au kufanya kazi kwenye makampuni makubwa. Wanashindwa kuelewa kwamba watu ambao wanamafanikio wanaishi kwa kutegemea kupata pesa kama kawaida.

Njia ya kuwa huru kifedha haitokani na kipato unachokipata bali ni ule uwezo wa kufanya na kufikiri kuhusu pesa.

Kwenye Makala hii nitakushirikisha  mambo matatu muhimu na mawazo sahihi kuhusiana na kuweza kuwa milionia. Kuweza kufanikisha mambo hayo sio tu  kwamba ni uhakika wa kuwa milionia, lakini ni njia za uhakika za kufanya maamuzi yalio sahihi.

1.           Jifunze Tofauti Kati Ya Mali Na Madeni
Nadhani ninapoongelea maana ya mali utakuwa unanielewa. Mali Inaweza kuwa vitu kama Nyumba, Uwekezaji na  Fedha zinazoweza kukuongezea thamani.

Chukulia mfano unataka kunua gari. Gari kwa kiasi Fulani inayo thamani lakini jiulize gari ulilonunua linakuingizia shilingi kwenye mifuko yako? Kama haiwezi kukuongezea pato lako basi hiyo hatuwezi kuita mali bali gari hilo tunaweza kusema ni deni kwako kwa sababu linapunguza pesa kwenye mifuko yako.

Kama gari hilo unalitumia kama daladala au taxi basi tunaweza kuliita ni mali kwa sababu linatengeneza pesa kila siku.

Unapoweza kufikiria kwa mtazamo huo utagundua kwamba matumizi ya pesa yako yanatakiwa yatumike pale ambapo pesa inaweza kuzalisha.

2.           Tambua Njia Za Kuzalisha Mapato
Watu wengi wanapatia maisha kutokana na kufanya kazi. Kufanya kazi ni njia ya uhakika ya kuzalisha kipato. Ni lazima ufanye kazi kila siku kama unataka kuzalisha kipato. Unaposimama kufanya kazi basi utakuwa umesimama kutengeneza pesa.

Utajiri wako unategemea ni kiasi gani unajituma kufanya kazi.

Kwa watu wengi kuzalisha mapato ni suala rahisi la kufanya ambalo hufanywa kwa kuwekeza pesa. Kuwekeza kwenye hisa ni uwekezaji mzuri kwa sababu hauhitaji uwepo wako wa moja kwa moja. Milionia wengi wanakuwa na vyanzo mbali mbali vya kuongeza kipato.

Kumbuka uwekezaji sio lazima uwekeze pesa. Bali pia unaweza kuwekeza muda. Kutengeneza biashara ambayo ina uwezo wa kujiendesha wenyewe, kama tovuti, ambayo inahitaji kazi kidogo. Kazi inapokamilika inakuwa inaendelea kwa kutumia mfumo ambao unajiendesha wenyewe.

3.           Ishi Chini Ya Njia Yako.
Haijalishi kwamba unatengeneza kiasi cha milioni mia moja kwa mwaka au milioni moja kwa mwaka, jambo la muhimu ni kwamba unaishi maishi ya kawaida. Usiwe kama wale watu ambao wanatumia tabia ya asili ya kuwa na matumizi makubwa pale ambapo wanapata pesa nyingi. Kumbuka kujenga tabia ya kutunza pesa Zaidi unavyoweza. Hata kama unapata laki moja kwa mwezi , unaweza kuanza.

Wakati mwengine mapato yako yanaweza kuongezeka, na hiyo ndiyo iwe njia ya kuongeza uwekezaji wako. Jaribu kuongeza fedha inayoongezeka kwenye akiba yako, badala ya matumizi hakikisha unaboresha maisha yako.

Hakikisha unajifunza na kufuata njia hizi zitakazo kuvuusha kufikia milionia. Jifunze tofauti kati ya mali na madeni, Tambua njia za kuzalisha mapato na Ishi chni ya njia yako. 
 
Weka email yako hapa na bonyeza NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA