Habari za leo ndugu msomaji wa nyota
ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za
kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala unayotakiwa kujifunza kutokana na mambo
yanayorudisha nyuma na makosa unayoyafanya.
Jinsi tunavyoweza kumudu hali
ngumu kwenye maisha ndivyo tunavyopata sura yenye kutuonesha vile tulivyo.
Namna tunavyoiangalia hali ngumu inayotutokea ni jambo muhimu katika
kushuhulikia makosa.
Uvumilivu na upendo ni kiungo muhimu
sana katika kuyafikia mafanikio. Kuwa na sababu ni muhimu vile vile pale
tunapokutana na mambo yanayorudisha nyuma. Unapoweza kukutana na makosa ni
wakati mzuri wa kupata uzoefu.
Kuna msemo wa zamani unaosema
kwamba mlango mmoja ukifungwa basi mwengine hufunguliwa. Kama kuna sehemu
umekwama lazima kutakuwa na fursa kwenye eneo jengine. Jambo la msingi ni kuwa
macho. Kuna watu ambao wanashindwa kuona fursa hata kama mlango utakuwa
wazi.
Pale mambo yanapokwenda kinyume
unatakiwa kujifunza jinsi ya kubaki kwenye kufikiri kwa muda na kuendelea
kubaki kwenye njia ya kutafuta ufumbuzi. Matatizo unayokutana nayo yanaweza
kuwa ya muda mfupi kama utaelekeza juhudi zako katika kusonga mbele. Hakuna
binaadamu ambaye hana matatizo , lakini tofauti ya kushinda na kushindwa
kutatua matatizo inatokana na ile hali ya kubaki kwenye njia iliyo
sahihi. Ili uweze kushinda ni lazima ubaki njia chanya na kuwa na msukumo
wa kwenda mbele.
Unapoamua kufanya lazima
utarajie matatizo. Unapoamua kutatua makosa na mambo yanorudisha nyuma ni
muhimu kuendelea bila ya kusimama na kukata tamaa.
Njia moja ya kuepuka makosa ni
kutambua kwamba yanaweza kutokea kila siku. Jambo la msingi ni kujiandaa bila
kusita. Matatizo, Makosa, Mambo yanaorudisha nyuma na kupoteza yote hayo ni
sehemu ya maisha. Hayo ni mambo ambayo hatuna budi isipokuwa kukubaliana nayo.
Hutakiwi kupata mshituko pale yanapokutokea.
Muhimu ni kuelewa kwamba
unapofanya makosa hurudii kosa lile lile. Tambua muda gani unatakiwa kuacha na
ni muda gani unatakiwa kuendelea mbele.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena