Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na Imani za pesa
zitakazokufanya ufe maskini.
Pesa Inatenganisha Familia. Umeshaona
mtu anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kusaka pesa. Muda wa kukaa na
familia unakuwa mdogo. Muda unapokuwa mdogo na mahusiano ya kukaa karibu na
familia yanapungua.
Watu wanaweza kukulaumu kwa
ajili ya kuitenga familia. Kwa sababu hii wewe unaweza kukata tamaa ya kutafuta
pesa, matokeo yake unaamua kuacha kujishuhulisha sana na kubaki na njia yako ya
umaskini. Ili uweze kuipata pesa ni lazima ufanye kazi sana, ni lazima ujitoe
sana na ni lazima familia na watu wako wa karibu wakubali kwamba pesa ndiyo
msingi wa mafanikio yenu. Badilisha Imani hii hatari na kuwa karibu na mawazo
ya pesa ili uweze kufanikiwa.
Hujui Kitu. Mfumo wetu
wa elimu unatuangusha sisi katika mtazamo wa pesa. Unatufundisha kuajiriwa na
kupata kazi mzuri. Unashindwa kutufundisha sisi jinsi ya kupata pesa na namna
ya pesa inavyofanya kazi. Unashindwa kutufundisha namna ya kuendesha biashara.
Kwa hivyo ni juu yako kujifunza
yote hayo. Jifunze kutafuta pesa, jifunze kuendesha biashara na jifunze kuwa
tajiri. Jiandae kwa kusoma vitabu vya pesa mara kwa mara. Unapotafuta maarifa
ya pesa utaanza kubadilisha Imani yako kuhusu pesa. Mafanikio yako na utajiri
yanaweza kukuwa haraka kama utakuwa na nia ya kuboresha.
Lawama. Watu
ambao ni maskini wanapenda lawama zao kuwapelekea watu wengine. Wenye mafanikio
wanakubaliana na lawama zao na wanakubali makosa yao, na kuchukua hatua za
kuboresha makosa yao.
Kuweza kupata fedha Zaidi na
mafanikio katika maisha yako, kwanza fanya uamuzi wa kutupa nje Imani hizi
mbaya. Kuwa tayari kukubali Imani mpya ambazo ni mzuri kwa malengo yako.
Unapoanza kujifunza mafanikio ya kupata pesa ndivyo unavyoweza kupanua uelewa
wako kwa kile kinachowezekana.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena