Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na Imani za pesa
zitakazokufanya ufe maskini.
Katika Ulimwengu watu tunatafuta
pesa kwa ajili kututumikia. Wewe ndiye bwana wa pesa na pesa ni mtumishi wako
muaminifu.
Hizi hapa ni Imani mbaya kuhusu
pesa na hatua za kuchukua kuondokana nazo.
Pesa si kila kitu. Baadhi ya
watu wanaamini kwamba pesa haziwezi kunua furaha. Lakini fedha ni kiashiria cha
mafanikio. Maskini na watu ambao hawana mafanikio wamekua na Imani hii na
kuwafanya wasifanye vitu vyenye maendeleo na hivyo kupelekea kushindwa kwa
upande mwengine. Watu wenye mafanikio wanakuwa na tabia zinazowaendeleza
kutimiza malengo na ndoto zao.
Hujui Jinsi Ya Kupokea. Watu
wengi tunashindwa kujua thamani ya kile tunachokitoa. Mfano mzuri chukulia wewe
umeweza kujifunza kitu kwa miaka mitano baada ya hapo ukawa na ujuzi wa kuweza
kuyafanyia kazi yale uliyojifunza. Jee unaweza kuipima thamani ya kazi
unayofanya au huduma unayotoa kwa malipo unayoyapata. Jibu ni hapana kwa sababu
muda uliotumia ni mwingi lakini ujira utakaopata naamini hauwezi kulipa elimu
yako. Na hii ni changomoto kwa watu wengi. Kutokujua thamani na jinsi ya
kupokea kunawafanya watu wafe wakiwa maskini.
Kukosa Kushukuru Kwa Kile
Ulichonacho. Anza kuwa na shukurani kwa kiasi
chochote cha pesa unachokipata. Shukurani ndio mzizi wa akili, ambao unakufanya
upokee na upanue mawazo yako. Na unapokuwa na shukurani uwezekanao wa kupata
mafanikio unaweza kuwa mkubwa.
Una Taswira Ya Kimasikini. Unaweza
kukua kama taswira yako ni ya kukua. Kama unataka kufanya tathmini kuhusu kazi
unayotaka kuifanya basi wewe unatakiwa kuwa wa mwanzo kuamini kwamba unaweza.
Ukijiwekea taswira hasi na Imani hasi kwamba huwezi basi wewe utakuwa mtu wa
kwanza kujitengenezea sumu yako.
Mara tu unapojenga Imani unakuwa
umejiletea thamani yako ambayo itakufanya ikupe nguvu za kuwa na furaha, afya
njema na kuweza kuendelea kufanya vizuri katika maisha yako.
Kuweza kuleta fedha Zaidi na
mafanikio katika maisha yako kwanza kabisa ni kufanya uamuzi wa kutupa nje
kabisa Imani hizi mbaya. Kuwa tayari kukubali Imani mpya ambazo ni mzuri kwa
malengo yako.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena