Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na nguzo muhimu za uongozi.
1.
Ushawishi. Kiongozi
Lazima awe na ushawishi. Kama huna ushawisi ni vigumu kuwaongoza wengine. Ili
uweze kuwa na ushawishi lazima uwe na tabia mzuri, Lazima uwe na mahusiano
mazuri na wale unaowaongoza, Lazima uwe na ujuzi wa kile unachoongoza, lazima
uwe na uzoefu wa kuongoza, Lazima uwe na uwezo.
2.
Unahoza. Kionngozi
ni mtu anayeona Zaidi kuliko mtu yeyote nyuma yake. Ni mtu anayeona mbali Zaidi.
Kiongozi anajua safari yote anayotaka kwenda kabla hajafika. Anafahamu nini
afanye ili aweze kuwafikisha watu wake salama.
3.
Uaminifu. Kiongozi
lazima awe ni mtu anayeweza kuaminiwa na jamii. Kiongozi huwa na sifa ya
kuongea kwa uwazi. Tabia ndio itakayokufanya uaminiwe. Maneno yako ya ukweli na
uwezi ndio itakayokufanya uwe kiongozi bora.
4.
Heshima. Watu
wanapokuheshimu wewe kama kiongozi watakufuata kwa jambo lolote
unatakalowaelekeza. Unapowapa watu heshima kama kiongozi watu vile vile
watkuheshimu.
5.
Kiongozi Anaunganisha Watu. Kiongozi
huwa anagusa nyoyo za watu kabla hajaulizwa kufanya hivyo. Ili kuweza
kuwaunganisha watu ni lazima ujitambue. Kiongozi mwenye sifa ya kuongoza watu
anakuwa uwezo wa kuwasilana na watu wake kwa uwazi. Kiongozi mzuri ni yule anayejua
watu wake kwa majina. Kiongozi bora anakuwa karibu na watu wake. Kiongozi
mwenye sifa anatoa maelekezo na kuwapa watu wake matumaini.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena