Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na kutengeneza taswira ya
mtazamo chanya kwa ajili ya maandalizi ya maisha bora.
Moja ya mambo muhimu ambayo
yanaweza kukupa fursa ya mafanikio yako na furaha ni jinsi gani unaweza kuona
taswira ya kivuli chako. Ukiwa na taswira chanya ni rahisi kuwa na nguvu ya
kukabiliana na changamoto za maisha. Hata kama mambo yatakuwa magumu unajua
kwamba unaweka maslahi na thamani yako kwanza katika mambo ambayo yanakuwa na
mtazamo chanya katika moyo wako. Kuwa na taswira ya mtazamo chanya
kutakujengea sifa kwa watu wako wa karibu na pia unakuwa umejitengenezea njia
ya kushi maisha bora.
Kuwa Na Ujasiri Wa Kusimama Na
Maamuzi Yako Mwenyewe
Unapokuwa na picha yenye taswira
ya mtazamo chanya kwenye akili yako, utakuwa umeweza kusimamia maamuzi yako.
Jiamini wewe mwenyewe na kuwa na Imani katika uwezo wako ulionao na fanya
maamuzi mazuri. Hali hiyo itakujenga katika kusimamia kitu ambacho unafikiri
kwako ni sahihi kufanya.
Wakati unapoamua kufanya maamuzi
iwe ni kwenye kazi, nyumbani au kwenye mahusiano yako na kama taswira ya mtazamo
wako iko imara unaweza kujisikia salama zaidi na kupata matumaini katika maisha
yako. Na hii inaweza kukupa nguvu na ujasiri wa kufanya kazi kwa bidii. Vile
vile hii italeta ndoto zako kuwa za kweli.
Ukiweza kuishi kwa kufuata
taswira halisi ya muonekano wako kuna uwezekano mkubwa wa kuishi kwa kufuata
maadili na malengo , ambayo ni msingi mkubwa kwa ridhaa ya baadaye na kuridhika
na maisha.
Ukiwa na Mtazamo Chanya Hutoweza
Kuhofia Kushindwa
Kama utaweza kuwa na fikra za
mtazamo chanya si rahisi kuwa na hisia za hofu kwenye kushindwa. Ukiweza kuwa
na nguvu za mtazamo chanya ni rahisi kushinda.
Ishi kwa kuwa na mtazamo chanya
na kuwa jasiri wa kusimamia maamuzi yako.
Weka email yako hapa na bonyeza
Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena