Jumanne, 8 Novemba 2016

Mafanikio Yanatengenezwa Haijalishi Ni Wapi Umeanzia


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na Mafanikio unayoweza kuyapata kwa kuanzia na hali uliyonayo sasa.

Mara nyingi tunawaangalia watu waliofanikiwa na kuona kama wana bahati. Ukweli ni kwamba watu waliofanikiwa wanatumia juhudi na maarifa kuweza kuleta mafanikio. Kuna mambo mengi ya msingi ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa wanamafanikio waliofanya vizuri duniani.

Uchaguzi wa kuishi maisha unayoyataka yako ndani ya uwezo wako. Unaweza kuendelea kuchagua vitu vibaya viendelee kuumiza kichwa chako ama kufanya mambo mazuri yatakayobadili maisha yako.

Uamuzi Ni Ufunguo Wa Maisha Yako. Uamuzi ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako lakini mara nyengine tunaona mambo ni magumu na kushindwa kubaki kwenye maamuzi mazito unayotaka kufanya kwa sababu tumezoea kufanya kwa kutegemea mteremko. Lakini kama una lengo na ndoto ni muhimu kufurahia hatua ndogo za mafanikio unayoyapata. Endelea kusonga mbele hata kama hujusikii kufanya hivyo. Uamuzi ndio nguvu yako ya kuyafikia malengo yako katika maisha.

Wasaidie Wengine Kuwa Na Maisha Mazuri. Unapoweza kuboresha ustawi na furaha kwa watu wengine ni sababu muhimu ya wewe kupata furaha pia. Zingatia kwamba upendo na msaada unaanzia nyumbani kwako kwanza, marafiki , majiranii na jamii kwa ujumla. Ni muhimu kutenga muda wako kwa ajili kusaidia mahitaji ya wengine, na hii itawafanya watu wajisikie bora na kukufanya wewe kuwa na mafanikio.

Kumbuka mafanikio ni kile ulichoweza kufanya bila kujali umeanzia wapi. Anza sasa popote pale ulipo. Amua na Ishi kwa kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.

Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA