Jumatatu, 7 Novemba 2016

Jifunze Mambo Haya Matatu (03) Uweze Kuishi Maisha Bora


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo matatu ya kujifunza ili uweze kuishi maisha bora.

1.           Jifunze Kutokana Na Hali Unayopitia
Maisha unayopitia usifikirie kwamba hakuna njia nyengine ya kukutoa hapo ulipo. Hali yoyote unayopitia ya maisha inaweza kuleta mafanikio. Hivyo jifunze kutokana na hali yoyote unayoweza kukukabili. Na usifikirie kwamba siku zote utapata matokeo mazuri katika maisha yako, bali hali inapokuja kinyume ichukulie kama somo la kujifunza katika maisha yako.

2.           Kuwa Bora Kuliko wote
Usiishi kwa kujisikia vibaya kwa kujilinganisha wewe na wengine, kila mtu ni wa kipekee na ni muhimu kufanya vizuri kuliko watu wengine.

3.           Kila Tatizo Lina Suluhisho
Unapopata tatizo ni muhimu kulitatua haraka, Unapoweza kutatua tatizo kwa haraka ndivyo utakavyojisikia Amani.  

Muhimu; Jifunze kutokana na hali unayopitia, Kuwa bora kuliko wote na tambua kwamba kila tatizo lina suluhisho.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.

Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA