Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana mambo matatu ya kuachana nayo
ili uweze kudhibiti maisha yako.
Hakuna jambo zuri katika maisha
kama kuishi kwa kutegemea masharti na misingi yako mwenyewe. Katika kuishi
maisha yako ni muhimu kuzingatia uzibiti wa maisha yako. Kuishi kwa kuchagua
njia yako ya maisha na kuishi kwa kufuata maadili yako ni jambo litakalokupa
faraja kubwa katika maisha yako.
Yafuatayo ni mambo matatu
unayotakiwa kuachana nayo ili uweze kudhibiti maisha yako:
1.
Achana Na Kuishi Kwa Kutegemea
Maisha Ya Mtu Mwengine
Kuishi kwa kutegemea maisha ya
watu wengine ni kama umekabidhi nguvu na akili yako mikononi mwa watu
wengine. Unapotegemea maisha ya watu wengine ni sawa na kuuza uhuru wako
binafsi na kutapelekea kuonekana kwamba wewe huko sawa kabisa. Jitambue kwamba
wewe ni wa peke yako na una uwezo wa kudhibiti maisha yako. Chagua maisha unayotaka
kuishi na ishi kwa kujiamini bila ya kutegemea maisha ya mwengine.
2.
Achana Na Matarijio Yasiyokuwa
Na Uhalisia
Unapojipa changamoto kunaweza
kukuongezea thamani ya maisha yako na kukufanya uishi maisha yenye furaha.
Achana na dhana ya matarajio. Usiruhusu akili yako ijiambie kwamba kama
nitashindwa kufanya kitu hiki vizuri kwa nini najisumbua kufanya, Kama nitashindwa
kujifunza kitu hiki kwa nini niendelee kufanya.
Mawazo kama hayo hayawezi kukupa
udhibiti wa maisha yako badala yake yanaweza kukurudisha nyuma katika maisha
yako. Ushauri wangu ni kukuomba uendelee kujaribu kufanya na kupata ujuzi mpya
bila ya kujali kwamba unaweza kufanya vizuri au vibaya.
3.
Achana Na Kuanza Kujilaumu
Mwenyewe Pale Mambo Yanapokwenda Vibaya
Kila mtu anafanya makosa. Na huo
ndio ukweli kwamba hakuna aliye kamilika. Ili kufanya maendeleo katika maisha,
lazima kuchukua hatari, Na unapofanya mambo ya hatari usiogope kushindwa. Kama
unataka kuchukua udhibiti wa maisha yako na kuanza kuangalia mbele, ni muhimu
kuacha kujilaumu kwa kuangalia makosa ambayo umewahi kuyafanya nyuma. Jiulize
ni kipi cha kujifunza kutoka kwenye mambo yaliyopita na fanya juhudi ya
kuangalia kufanya vizuri zaidi baadaye.
Sio jambo rahisi kudhibiti
maisha yako na ndio maana walio wengi wanashindwa njiani, lakini kuchukua hatua
na kuanza njia mpya ya maisha ni thamani kubwa katika kuboresha maisha yako.
Hivyo kuanzia leo achana na maisha tegemezi na ishi maisha yako, Achana na
matarajio yasio na ukweli na achana na kuanza kujilaumu wewe mwenyewe kwa
makosa yako unayoyafanya. Chukua hatua leo ili maisha yako yawe na mafanikio.
Weka email yako hapa na bonyeza
NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
0784498867
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena