Ijumaa, 4 Novemba 2016

Zijue Njia Sahihi Za Kupanga Muda Wako Vizuri Kwa Mafanikio Ya Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana Njia sahihi za kupanga muda kwa mafanikio ya  maisha yako.

Watu waliopata mafanikio makubwa ni watu ambao wanajituma katika kuyasaka mafanikio. Waliopata mafanikio hawakupata kwa bahati mbaya, bali walifanya maandalizi ya kutosha, walipanga mipango yao vizuri na waliweza kuupangilia muda wao vizuri kwa kufanya yale mambo ambayo yana umuhimu kwao.

Hizi hapa ndio njia ambazo watu waliofanikiwa wanazitumia katika kupanga muda wao vizuri:

1.           Wanahifadhi Maamuizi Yao Katika Kufanya Mambo Muhimu.
Mara nyingi tunapata kuona watu wenye mafanikio ni watu ambao wanarahisisha mambo yao. Ni watu ambao wanapunguza kufanya maamuzi kwenye mambo yasiyo ya muhimu kwao. Watu hawa hawana muda wa kupoteza wa kufikiria kwamba watakula nini au watavaa nini. Ni watu wanaofanya mambo yao kwa muda walioupanga. Wanafahamu uwezo wao na kukazana katika kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na athari katika maisha yao.

2.           Wanaendesha Mambo Yao Kwa Kufuata Ratiba Ya Asubuhi.
      Ili uweze kupanga muda wako wa siku vizuri, ni lazima siku yako uianze asubuhi. Watu walioweza kuleta mafanikio kwenye maisha yao wanaianza siku kwa Kusoma, Kufanya Mazoezi, Kufanya Tahajudi, Kuweka kipaumbele mambo ambayo ni muhimu kwa mafanikio ya maisha yao. Wanahakikisha mambo yote muhimu ya siku wanayaanza kuyafanya asubuhi. Watu waliofanikiwa wanatengeneza ratiba maalumu ambayo huweza kuifanyia kazi kila siku asubuhi wanapoamka.

3.           Wanafanya Maandalizi Ya Mipango Yao Usiku.
Kumbuka kabla hujafanya kitu chochote maandalizi ndio msingi wa mafanikio yako. Usisisubiri mpaka siku iingie ndio ufanye maandalizi. Ni muhimu kupanga siku usiku kabla ya siku husika. Ukipanga siku usiku, unapoamka utaona kila kitu kinakwenda vizuri.

4.           Wanapanga Mipango Ya Baadaye.
Moja ya tofauti kubwa kati ya watu wenye mafanikio na ambao hawana ni kwamba wenye mafanikio wanafikiria kwa kina kuhusiana na mawazo na mipango wanayotaka kufanya. Hii inawafanya kufanya maamuzi sahihi.

5.           Wanaweka Kipaombele.
Watu waliofanikiwa wanatambua kwamba kama hawajaweka kipaombele kwenye mambo wanayoyafanya ni rahisi kufanya mambo ambayo hayako kwenye malengo. Vipaombele ndivyo vinavyowafanya waweze kutumia muda wao vizuri na kuweza kufanya mambo ambayo ni ya lazima.

 
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA