Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na bosi wa maisha yako.
Kuanzisha biashara yako inaweza kuwa ni mojawapo wa uzoefu unaoweza kuupata kwenye maisha yako. Kwa mara ya kwanza unaweza kuona ni jambo gumu sana lakini kadiri unavyoendelea kukua unaweza kufurahia mafanikio makubwa utakayoweza kuyapata.
Ni jambo zuri kwenye maisha yako kuanzisha biashara yako mwenyewe na kufanya kazi zako na si kufanya kazi za kuajiriwa. Kabla hujanza biashara yako kuna mambo ya msingi lazima uyazingatie. Mambo hayo ni pamoja na kujua faida za kuwa bosi wa maisha yako na njia za kufanikwa kama mjasiriamali.
Faida ya Kuwa Bosi wa Maisha Yako
Wakati unafikiria kuwa bosi wa maisha yako, jambo la kwanza linatakiwa lije kwenye akili yako ni uhuru wa maisha yako. Unaweza kupanga muda wako mwenyewe na kufanya kazi kwa uhuru wa hali ya juu na hakuna mtu anayeweza kukupangia muda wako. Bila ya shaka kuna faida nyingi lakini faida kubwa ni kwamba unakuwa umeachana na utumwa.
- Unaweza Kuokoa Fedha. Unapomudu kuweza kufanya kazi zako mwenyewe kuna uwezekano wa kuokoa pesa nyingi sana. Ni rahisi kuacha kufanya mambo ambayo hayana faida kwako na kufanya mambo ambayo yanaweza kukuingizia pesa.
- Unakuwa na Uhuru wa Kuchagua Kufanya Unachokitaka. Unapofanya kazi za utumwa unakuwa unafanyakazi za kurudia rudia. Kila siku unafanya kazi zile zile. Uwezo wako wa akili unadumaa. Unapoamua kuwa bosi wa maisha yako unakuwa unafanya kazi zako unazotaka kufanya, hakuna wa kukuwekea mipaka.
- Njia Za Kufanikiwa Kuwa Bosi Wa Maisha Yako
Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi unayoyotakiwa kuyazingatia kabla hujawa bosi wa maisha yako. Kuwa bosi wewe mwenyewe ni zawadi lakini ni muhimu kufahamu njia sahihi za kupita. - Fahamu watu unaowalenga. Kitu cha kwanza ni kuelewa wateja wako. Elewa wateja wako wa bidhaa au huduma unazotowa. Jifunze wateja wanataka nini, chunguza soko lako, tengeneza mbinu zitakazowafanya wateja wavutiwe na biashara yako. Ni muhimu kufanya uchunguzi wa soko na kujua washindani wako wa biashara.
- Unda Uwepo wa Tarakimu. Baada ya kuwafahamu wateja sasa ni wakati wa kulijua soko. Ili uweze kulijua soko vizuri inakulazimu uweze kufahamu uwepo mkubwa wa tarakimu. Tarakimu nina maana ya kucheza na hesabu ya hali ya juu. Bila ya kuwa na hesabu mzuri juu ya masoko unaweza kuanguka.
- Jiandae na Chochote Kinachoweza Kukutokea. Kuwa tayari kwa hali yoyote inayoweza kujitokeza. Kama itakuwa mbaya jiandae na mpango mwengine. Fanya maandalizi kwa jambo lolote utakalokutana nalo.
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena