Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo makubwa yanayoweza
kukuvuusha kwenye mafanikio.
Ni mara nyingi tumeona watu
wakitengeneza lawama kwa kila mtu anapofanya makosa. Ili tuweze kutimiza
malengo yetu, hatuhitaji kuishi kwa kutegemea kwamba wewe uweze
kuwashinda watu wote. Kwenye maisha kila mtu ana mapungufu yake, hivyo
usichukulie uzaifu wao kama silaha yako ya kuwahukumu wengine. Kama tutaangalia
mtazamo wa maisha ni vyema kuangalia udhaifu wako kuwa ndio kigezo sahihi cha
kuimarisha mafanikio yako.
Haya hapa ndio mambo ambayo
ukiyafanya yatakupeka kwenye mafanikio unayoyataka.
1.
Tengeneza Mfumo Wako Wa Maisha
Tengeneza mfumo ulio imara ambao
utakuwezesha kuishi maisha yako. Jifunze uwezo wa kuwa jasiri wa kufuata
mapenzi na hisia zako zinavyokuongoza. Tengeneza hadithi ya maisha yako. Na
kuweza yote hayo ni lazima ukubali kwamba uzaifu wako ndio nguvu yako ya
kuimarisha mafanikio yako.
2.
Kufeli Ni Mwalimu Mzuri
Watu walioshinda kwenye maisha
yao walifanya kazi ngumu ya kutafuta mafanikio, lakini pia walipuuzia
kushindwa. Waliweza kuwa wajasiri na hawakukata tamaa. Ni muhimu kuelewa kwamba
kufeli ni mwalimu mzuri. Huwezi kufanikiwa bila ya kupitia njia ya kufeli. Na
huwezi kufanikiwa kama hujajifunza kotokana na kufeli. Kuwa na muda wa kutosha
wa kuweza kujifunza kutokana na makosa unayofanya.
3.
Jiwekee malengo Makubwa
Malengo na mipango yako
unayopanga katika maisha ni muhimu yawe makubwa. Kama unataka kupata mara kumi
basi ni vyema kupanga kupata mara mia moja. Ukipanga kupata mambo makubwa
kutakusaidia kutimiza ndoto zako. Unaweza kufanya kazi kwa bidii na kufanya
kila njia ili kuweza kufikia malengo yako. Unapopanga kufanya mambo makubwa
hutoweza kuogopa kushindwa. Ukiweza kuweka ndoto kubwa utafanya kila
linalowezekena kufanikisha na kutafuta uzoefu wa kutosha.
Weka email yako hapa na bonyeza
Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena