Jumanne, 1 Novemba 2016

Makosa Matano (05) Ya Kuepuka Kama Unataka Kufikia Malengo Na Ndoto Katika Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na makosa unayotakiwa kuyaepuka ili uweze kufikia malengo na ndoto zako katika maisha.

Haijalishi umejiwekea malengo yenye ukubwa gani au udogo kiasi gani, lakini ukweli ni kwamba unahitaji dhamira, lengo, kufanya kazi kwa bidii, ujasiri na uamuzi wa kufanikiwa. Hakuna njia ya mkato yenye matumaini ya kuleta mafanikio kwenye malengo yako bila ya kupitia mambo haya muhimu. Watu wengi linapokuja suala la malengo huwa tunafanya na tunapofika njiani tuacha kufanya kwa sababu ya ugumu wa kufanya.

Unapoamua kuianza safari yako ya mafanikio epuka kufanya makosa haya matano ili uweze kuongeza nafasi yako ya kufikia ndoto na lengo ulilojiwekea katika maisha.

1.           Epuka Kutarajia Matokeo Ya Haraka
Kosa hili linaweza kuwa na athari kubwa kwenye Imani yako na matarajio ya kufanikiwa. Kama unaweza kutarajia matokeo ya haraka kinachotokea ni kupoteza dira na muelekeo wa kufikia ndoto na lengo lako ulilojiwekea. Linapokuja jambo la malengo unahitaji kuwa na uvumilivu wa hali ya juu. Uvumilivu wako ndio utakaokufanya kutimiza safari yako ya mafanikio.

2.           Epuka Kuwa Na Mtazamo Wa Kushindwa
Ni kosa kubwa kukubali kwamba umeshindwa zaidi ya mara moja na kwamba sasa huwezi kusimama tena na kuanza upya.

Ili uweze kujimudu kwenye maisha yako ni pale unapokabilana na kushindwa. Ni wewe ndiye utakayeamua ni jinsi gani kushindwa kunaweza kuathiri maisha yako. Unaweza kuamua kushinda au uamue kukata tamaa.

3.           Epuka Kushindwa Kwa Kutarajia Au Kupangilia Yasiyotarajiwa
Kwenye malengo yetu tutarajie kupata ambayo hatujatarajia kuyapata. Ni kawaida kwetu tunapokutana na mambo ambayo hatujayatarajia tunaona kwamba kila kitu kimeshakuwa hakiwezekani. Njia mzuri ya kufanya tunapopanga malengo yetu ni kufanya maandalizi kwa ajili ya mambo tusiyoyatarajia.

4.           Epuka Kuchoka Njiani  
Kwa ajili ya kupata kile unachokitaka kwenye maisha yako ni lazima ubadilike, fanya vitu kwa utofauti, tengeneza tabia mpya na mawazo mapya. Na vyote hivyo haviwezi kuja kwa usiku mmoja. Vitu hivyo vinatokea kwa kuendelea kuvirudia kila siku. Jiandae na hali itakayojitokeza ya kutokujisikia kufanya. Inapojitokeza hali hiyo ni muhimu kuendelea kila siku mpaka utimize ndoto uliyojiwekea.

5.           Epuka Kujilinganisha Na Wengine
Kitendo cha kujilinganisha maisha yako na wengine kitakufanya usiweze kufanya vyema katika malengo yako. Usichukulie kufeli kwa mtu mwengine kwamba na wewe ndio huwezi kufikia ndoto zako na malengo yako. Tambua kwamba watu hatulingani na inawezekana nyote mukawa na lengo na ndoto za aina moja lakini mafanikio yakawa tofauti kabisa.

Unapoweza kuepuka makosa haya matano utaweza kutimiza malengo yako, utakuwa na nidhamu mzuri, utaweza kuwa jasiri na utakuwa na msimamo utakaoweza kukusaidia kufanikiwa katika mambo yote ambayo unataka kufika katika maisha yako.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA