Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Mambo Manne (04) Unayoweza Kufanya Ili Kuwa Kocha Wa Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kuwa kocha wa maisha yako. 


Kila Mtu anahitaji kuwa bingwa. Maisha ni mchanganyiko wa heka heka na changamoto nyingi zinazoweza kukuzuiya wewe kuwa mshindi. Vikwazo kutokea ni jambo la kawaida katika maisha. Watu wengi wanapenda kutafuta makocha ili waweze kuwasaidia katika malengo yao. Lakini umewahi kufikiri kwamba wewe unaweza kuwa kocha mzuri kwenye maisha yako.

Hizi hapa ni baadhi ya njia ambazo unaweza kujifunza ili uweze kuwa kocha wa maisha yako na kuweza kukupatia mafanikio katika safari yako.

1.           Tambua Maeneo Ya Kuboresha
Pengine ulikuwa tayari na mawazo ya kutafuta kocha wa maisha yako au ulikuwa unafikiria ufanye nini ili kuboresha maisha yako.

Ili kuweza kutambua maeneo ya kuboresha, hatua ya kwanza unayoweza kuchukua ni kujitafakari wewe mwenyewe, kuwa mwaminifu kuhusiana na maeneo unayotaka kuboresha. Pengine unataka kuboresha afya yako kwa kufanya mazoezi au unataka kuboresha mambo yako yanayohusu pesa kwa kuweka mikakati ya kupanga bajeti vizuri, au unataka kufanya maboresho kwenye kazi unayofanya.

Chochote unachotaka kuboresha katika maisha yako, tengeneza orodha itakayolenga kufanya eneo moja kwa wakati mmoja.

2.           Tambua Changamoto Zako
Wakati unahitaji kuzingatia uwezo wako wa kufanya mabadiliko katika maisha yako, ni muhimu kutambua changamoto unazokutana nazo. Kutambua changamoto zako kutaweza kukusaidia kuendeleza mpango kazi wako. Tambua watu wote wanakuwa na changamoto, lakini mikakati sahihi ya kutatua changamoto hizo ndio inayompa mtu uwezo wa kushinda. Na hapo ndipo utakapoweza kuwa kocha wa maisha yako. Kazi yako hapa ni kuonesha uaminifu wa nafsi yako na kubaki na njia ya kuwa unaweza kufanya. Tambua udhaifu wako na fanya mabadiliko mara moja kuhusiana na mambo unayoyataka.

3.           Jielimishe Mwenyewe
Akili yenye elimu ni akili yenye nguvu. Fanya utafiti na jifunze mbinu mbali mbali unazoweza kuzitumia katika maisha yako. Kama wewe ndiye kocha wa maisha yako jifunze kila eneo unalohitaji kulijua kwenye maisha yako. Kufanya hivyo itakupa manufaa kwako na kuweza kufanya mabadiliko makubwa kuhusiana na maisha yako.

4.           Jifunze Kutoka Kwa Wengine
Sikiliza au soma mambo mbali mbali kutoka kwa watu walioweza kufanya vizuri kwenye maisha yao. Na njia mzuri ya kupata mafanikio ni kuiga na kumfuata mtu ambaye tayari amefanikiwa. Uzuri ni kwamba watu wengi waliofanikiwa wamesaidia kutowa vidokezo na mbinu walizotumia kupata mafanikio.

Hata hivyo kwa ajili ya kutambua kwamba mahitaji yako ni tofauti na ya kipekee, bado unahitaji kusikia na kupata msukumo kutoka kwa watu waliopata mafanikio.

Kuwa kocha wa maisha yako kutakupa nguvu ya kuweza kutambua uwezo wako. Kutakupa motisha wa kuweza kufikia malengo yako. Kutakupa amani na furaha na kuweza kukuletea mwanga unaoweza kufanya watu wengine waone matokeo yako.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA