Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na utabiri wa mafanikio wa
maisha yako.
Tunapozungumzia mafanikio ya
maisha yapo mambo muhimu unayotakiwa kuyatimiza. Na sio tu kuwa na pesa za
kutosha lakini ni pamoja na kuwa na afya njema, kuwa na mahusiano mazuri na
watu pamoja na familia, kutimiza malengo yako na mambo mengine mengi ambayo
yanatufanya tuishi maisha tunayoyataka.
Haya hapa ndio maswali manne
ambayo yanatabiri mafanikio ya maisha yako.
1.
Je, Wewe Tayari Umejiandaa
Kiakili?
Watu wenye mawazo ya ukuaji
kwenye akili zao huona kushindwa kama ndio somo la uhakika ambalo linaweza
kumtoa kwenye kifungo cha umaskini na kumpeleka kwenye mafanikio.
Ni kawaida kwake kukubaliana na
changamoto, kuboresha misingi mbali mbali ya maisha yake ili aweze kufikia
malengo aliyojiwekea.
2.
Una Furaha?
Mtazamo chanya ni kiungo muhimu
kwa mafanikio na kukusaidia kukuweka katika hali ya furaha na kuweza kuwa na
matumaini mazuri. Kufurahia kila hatua unayoipiga kwenye maisha yako
kutakuongezea nguvu ya kuweza kupambana zaidi katika kuyafikia malengo yako
makubwa. Ili uweze kuwa na furaha lazima uwe na upendo na mahusiano mazuri kwa
watu.
3.
Je, Una Mapenzi Na
Unachokifanya?
Moja ya sababu muhimu ya
kufanikiwa kile ulichoamua kufanya ni kufanya kwa mapenzi ya hali ya juu.
Hakikisha unapata nguvu na msukumo wa kutaka kuendelea kufanya. Kila siku weka
uhakika wa kuboresha hatua nyengine zaidi.
Kama huna mapenzi na unachofanya
ni bora kuacha kufanya, kwa sababu ukiendelea kufanya ni kama unapoteza muda
wako. Ishi kwa kufanya yale mambo unayoyapenda.
4.
Uko Tayari Na Kukabiliana Na
Hatari Ya Kupoteza?
Watu ambao wamepanga malengo yao
ya kupata mafanikio tayari wanajua lazima watakumbana na hatari. Tayari
wameshaweka maandalizi ya kukabiliana na hatari hizo zinapojitokeza. Hivyo
hakuna kitu ambacho kitawafanya wawe na msongo wa mawazo kwao.
Kumbuka kwamba huwezi kuwa na
mafanikio makubwa kama utakuwa hujaweza kutimiza mahitaji yako ya lazima.
Mahitaji ya lazima ni kama chakula, mavazi na malazi. Kama umeweza kukamilisha
hayo ndio sasa unakwenda kwenye hatua nyengine ya mafanikio makubwa. Mafanikio
hayo yatapatikana kutokana na malengo na mipango imara uliyojiwekea pamoja na
kufuata utabiri unaokuongoza kuelekea kwenye safari ya mafanikio ya maisha
yako.
Weka email yako hapa na bonyeza
Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena