Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo matano muhimu kutoka
kwa wafanyabiashara wenye mafanikio.
Watu wengi ambao ni wafanyakazi
huwa wana mawazo na shauku ya kutaka kuanzisha biashara. Na changamoto kubwa ni
kuwa hawajui waanzie wapi ili waweze kufanikiwa katika biashara
watakazozianzisha. Unapoamua kuanzisha biashara unahitaji kujitoa kweli, na
lazima uweke mipango mizuri.
Uamuzi wa kuianzisha biashara ni
wa busara lakini ni vyema kujua mbinu bora zitakazoweza kufanikisha biashara
hizo. Kama umeamua kuingia kwenye biashara ni vizuri kujifunza na kusikiliza
ushauri kutoka kwa wafanyabiashara wenye ufanisi mkubwa wa biashara unayotaka
kwenda kuifanya.
Na huu hapa ndio ushauri mzuri
kutoka kwa wafanyabiashara waliofanikiwa kwenye biashara zao:
1.
Tumia Hekima Wakati Wa Kuchagua
Washiriki
Mtandao wa watu unaweza kuwa na
mchango mkubwa kwenye biashara yako. Chagua marafiki watakaoweza kukusaidia
kufanya vizuri katika biashara yako . Watu waliokuzunguka wana mchango mkubwa
katika biashara unayoifanya. Hakikisha watu uliowachagua wanakuwa ni watu wenye
malengo mazuri katika maisha yao.
2.
Kuwa Na Wawakilishi
Watu ambao wanatumia muda wao
katika kuweka juhudi zao kwenye kujenga biashara huwa wanakuwa wazito sana
linapokuja jambo la majukumu na kuwapa watu wengine. Ni vyema kwenye biashara
yako uwe na wajumbe watakaokusaidia katika kazi zako. Huwezi kufanya kila kitu
wewe mwenyewe. Kufanya kila kitu wewe utajipa mzigo mkubwa ambao unaweza
kushindwa njiani.
3.
Usiruhusu Kushindwa
Haijalishi unapitia magumu kiasi
gani, lakini lazima kutakuwa na njia nyepesi. Unapoona umeshindwa njia moja,
buni njia nyengine itakayoweza kufanya vizuri. Hata hivyo wajasiriamali wakubwa
duniani wanaamini kwamba hakuna linalishindikana kama umeamua kufanya jambo
kubwa.
4.
Wajue Wateja Wako Vizuri
Ni muhimu kuwajua wateja wako
kwenye biashara unayofanya. Biashara inajengwa na misingi ya kuweka akili na
mawazo yako katika kuwajua wateja wako. Wateja ndio watakaokufanya uweze kukua
kwenye biashara yako. Hivyo unapoamua kutengeneza bidhaa zingatia mahitaji ya
wateja wako.
5.
Usitosheke Na Ulipofikia
Siku zote jifunze mambo
yanayohusiana na biashra yako. Usipime mafanikio yako ya biashara kwa kuridhika
na kiwango ulichofikia. Hakikisha kila siku unaongeza thamani ya biashara yako.
Wafanyabiashara wenye mafanikio wamekuwa na mafaniko kwa sababu waliweza
kuzikuza biashara zao.
Ndugu msomaji wa makala hii
nakushauri uzingatie haya mambo matano kama kweli umeamua kufanikiwa kwenye
biashara uliyoanzisha.
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe
ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena