Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Makosa Makubwa Matatu (03) Wanayoyafanya Watu Wanaoshindwa Kufikia Mafanikio.


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na makosa makubwa wanayoyafanya watu wanaoshindwa kufikia mafanikio.

Katika ulimwengu wa sasa kila mwanaadamu anaishi kwa kutamani kuyafikia mafanikio.  Kwenye mafanikio kuna kupata na kukosa. Huwezi kufanikiwa pasipo na kutenda makosa, lakini makosa hayo ndio ngao kuu ya wanaadamu kufikia mafanikio kama watazingatia kanuni, ushauri na misingi sahihi ya maisha.

Haya hapa ndio makosa makubwa matatu ambayo watu wanashindwa kufikia mafanikio yao kama wataendelea kuyafanya:

1.           Kujiwekea Mipaka.
Ni kosa kubwa kujiwekea mipaka kwa jambo lolote lile. Badala yake ishi kwa kuwa na ndoto ya kupata zaidi ili mafanikio yako yawe makubwa zaidi. Kuwa na mipaka inaweza kuwa ndio chanzo cha majaribio mengi ya kushindwa katika mafanikio. Mipaka inaweza kutupa imani dhaifu kwamba hatuwezi kuyafikia mafanikio. Unapoamua kufanya bila ya mipaka utaweza kujenga misingi ambayo inaweza kukuongoza katika njia ya mafanikio.

Usitumie vikwazo ambavyo vinatokana na mipaka uliyojiwekea kama ndio njia moja wapo ya kukata tamaa. Ni jambo jema kutambua kwamba kwenye maisha hakuna kinachoshindikana.

2.           Hawajifunzi Kutokana Na Makosa Wanayoyafanya.
Katika maisha makosa hayawezi kuepukika. Mara nyingi makosa huwa yanawarudisha watu nyuma. Jifunze kwa kila kosa unalolifanya na ukifanya hivyo unakuwa umetengeneza njia yako ya mafanikio.

Unaweza kufanya makosa zaidi ya elfu moja lakini kama hurudii makosa unayofanya basi utakuwa umeweza kujifunza na umeweza kufanikiwa kukua. Watu waliofanikiwa hawafanyi kosa hili.

3.           Hawana Hamasa.
Hamasa ndio inayowasukuma watu kwenye mafanikio. Huwezi kufanikiwa katika kitu chochote kile bila ya kuwa na hamasa. Fanya bidii yako ya hali ya juu ili uweze kupata kile unachotaka. Tafuta vitu vinavyoweza kukupa hamasa zaidi kwenye lile eneo unalolifanya. Hamasa huibua nguvu ya kufanikisha lengo lolote la maisha. Hamasa inajenga ukomavu wa muendelezo wa kitu mpaka pale kinapotokea na kuwa uhalisia.

Ili uweze kupata mafanikio ya kweli katika maisha usirudie makosa hayo. Hakikisha hujiwekei mipaka kwa jambo lolote unalolifanya. Hakikisha unajifunza kwa kila kosa unalolifanya na mwisho lazima uwe na hamasa kwa kitu chochote ulichoamua kufanya. Ukiweza kutekeleza haya kwa muda mfupi unaweza kuyaona matunda ya mafanikio ya maisha yako.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA