Alhamisi, 27 Oktoba 2016

Hatua Tano (05) Unazopaswa Kuzifuata Kwa Ajili Ya Kuweka Mipango Mizuri Katika Kipindi Cha Miaka Mitano Ijayo.


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na kuweka mipango mizuri katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili uweze kufika safari yako ya mafanikio.

Miaka mitano inaweza kuonekana kama muda mrefu kama umeweka mipango na unajua nini unataka kufikia.  lakini bila mipango , miaka mitano inaweza kupita haraka sana.

Hizi hapa ndio hatua tano ambazo ukizifuata zitakusaidia kuwa na uhakika wa kuishi maisha bora baadaye:

1.           Amua Ni Nini Unataka Ufikie Ndani Ya Kipindi Cha Miaka Mitano Ijayo.
Amua nini unataka kupangilia ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo. Amua kama unataka kuanzisha biashara yako mwenyewe.

Mipango ni sehemu muhimu kwa kuhakikisha unapata kile unachotaka. Maisha yamejawa na matukio mengi ya uwezekano, hivyo lazima ufanye kazi kwa bidii ili kufikia kile unachotaka ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Chukua kalamu na karatasi na andika majibu ya maswali haya: Jee ni nini unataka kufikia? Ni muda gani lengo lako itachukua kulifikia?  Kitu cha kwanza nahitaji kufanya nini?

2.           Tathmini Malengo Yako Kila Mwezi.
Kama uliweka lengo lako wiki iliyopita au miaka mitano iliyopita ni muhimu kufanya tathmini ya mara kwa mara malengo yako. Maisha yako yanaweza kuwa yamebadilika au vipaumbele vingine huenda vimeibuka, hivyo hakikisha unazingatia mambo ya muhimu kwako katika kufanya tathmini ya kila mwezi. Kwa mfano umepanga kunua nyumba eneo fulani lakini mara ukabadilisha mawazo kutokana na mabadiliko yaliyotokea. Hivyo kaa chini mara moja kwa mwezi na andika majibu ya maswali haya: Jee lengo hili bado ni muhimu kwangu? Jee bado nina shauku ya kutaka kutekeleza wazo langu?

3.           Pitia Malengo Yako Kila Siku.
Watu wengi wana malengo, lakini watu waliofanikiwa zaidi huweka akili zao mbele kwenye malengo yao wakati wote. Ni muhimu kugawa malengo makubwa katika malengo madogo madogo. Hii itakusaidia kuhakikisha kila siku unafanya kitu kwenye malengo yako.

Jiulize kila siku: Ni vipi naendelea na malengo yangu? Ni kazi zipi naweza kufanya kwa siku ili kuweza kuwa karibu na lengo langu? Nifanye nini leo ili niweze kufikia malengo yangu ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo? Jee naweza kufikia malengo yangu mapema zaidi?

4.           Weka Ahadi Kila Wiki Kwa Malengo Yako.
Unapomaliza kuandaa malengo yako, kilichobaki ni muda wa kutekeleza. Tambua kwamba malengo yako unaweza kuyafikia kwa urahisi iwapo utaweza kuanza kazi mara moja. Leo ni wakati bora wa kuanza kuliko kusubiri kesho.

Mwanzoni mwa kila wiki, andika yale unayodhamiria kuyafanya kwa wiki hiyo, na hii ni kwa ajili ya kuelekea kufanikisha lengo lako. Sio lazima ufanye kitu kikubwa kila wiki, hata kufanya kitu kidogo kutakusaidia kuona kwamba unaweza kuelekea lengo lako la kila siku.

5.           Andika Matokeo Yote Yanayowezekana.
Chukua kalamu na karatasi na andika mambo yote ambayo unaweza kuyafanya ili uweze kukamilisha malengo yako. Wakati mwengine kutakuwa na changamoto za kutisha, lakini hiyo ndio njia nzuri kwako ya kutatua matatizo ya kuelekea safari yako.

Angalia njia za kufanya kwa ajili ya kuboresha kwa kila lengo, na mara kwa mara angalia majibu yako.

Huenda ukashindwa kudhibiti siku zijazo, lakini unaweza kudhibiti hali ya kukabiliana na maisha kutokana na njia uliyoichagua. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo unaweza kukabiliana na changamoto na matatizo mbali mbali, lakini watu waliofanikiwa zaidi waliweza  kukabiliana na hali hiyo kwa kutatua changamoto zao. Na mwisho waliweza kufika kilele cha safari yao ya mafanikio.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required
   

Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA