Jumatano, 26 Oktoba 2016

Fahamu Ishara Saba (07) Ambazo Zinakuonesha Mwanga Wa Mafanikio Wa Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na ishara zenye kuonesha mwanga wa mafaniko wa maisha yako.

Katika maisha ni jambo la rahisi kuona kwamba umeshindwa. Ni kawaida kwa mtu kuweza kuwa na hisia ya kushindwa. Kuna wakati unatokea tunapuuzia vitu vidogo. Unapojiona wewe kwamba hujafikia utajiri wa kuitwa milionia au huna gari zuri tayari unajenga hisia kwamba umeshashindwa, lakini ukweli ni kuwa mtazamo wako wa hisia hauko sahihi.

Fahamu kwamba katika maisha ya mafanikio zipo alama nyingi ambazo zinaweza kukuonesha mafanikio yako katika maisha.

Na hizi hapa ni ishara saba zinazokuonesha kwamba unaendelea kufanikiwa katika maisha:

1.           Umeweza Kupandisha Viwango Vyako.
Jambo lolote unalolifanya kwa sasa unalifanya kwa kuzingatia viwango vyenye ubora wa hali ya juu. Kwa sasa huwezi kuvumilia uovu wa watu wengine na wewe pia hufanyi maovu. Kama wewe unaongoza watu basi uongozi wako unawafanya watu waweze kuwajibika kwa vitendo kwenye kazi zao.

2.           Umeweza Kujifunza Kwamba Vipingamizi na Kushindwa ni Sehemu ya Ukuaji Wako.
Hakuna mtu aliyeweza kupata mafanikio asilimia mia moja pasipo kuwa na vipingamizi. Maisha ni kupata na kukosa. Hivyo ishi kwa kutambua kwamba vikwazo ni ishara ya kufanya vizuri. Uhalisia unaonesha kwamba hakuna kitu ambacho kinaweza kukurudisha nyuma kama umeamua kukua. Ukiweza kufikia kiwango hicho basi hiyo ndiyo ishara ya safari yako ya ushindi.

3.           Umeweza Kutengeneza Mfumo Wa Watu Ambao Wako Tayari Kukupa Msaada Wa Jambo Lolote.
Kama umeweza kutengeneza watu nyuma yako ambao wako tayari kukuona wewe unapiga hatua kwenye maisha yako. Watu hao wako tayari kwa hali na mali kuona maisha yako yanakamilisha ndoto zako, basi tambua kwamba hiyo ni ishara ya mafanikio.

4.           Wewe Sio Mtu Wa kulalamika.
Kwa sababu unajua kweli hakuna kitu kinachoweza kukufanya ulalamike. Kama wewe umeanza kuwa huna tabia ya kulalamika basi ujue kwamba hiyo ni ishara moja wapo ya mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki na wanaishi maisha ya amani.

5.           Unayo  Mambo Yanayokufanya Uangalie Mbele.
Kama huna kitu ambacho kinaonesha kwamba unasonga mbele kwenye maisha yako basi unajiua wewe mwenyewe pole pole. Watu waliofanikiwa wanatengeneza mipango na malengo inayowafanya wafikirie mbele.  Siku zote wanafikiria mambo ambayo yanawasukuma kwenda mbele kimaisha.

6.           Hujali Watu Wanavyo Kufikiria.
Unatambua kwamba huwezi kumfurahisha kila mtu. Unakuwa na ufahamu kwamba watu wanavyokuwa na mtazamo na mawazo tofauti kwa wengine hayana mashiko. Ukweli wako unaujua mwenyewe na hakuna mtu mwengine anayeweza kujua kuhusu wewe.

7.           Wewe Ni Mtu Wa Furaha.
Furaha ndio maana halisi ya mafanikio. Haijalishi una kiasi gani cha pesa kwenye akaunti yako, una nyumba kubwa au gari la kifahari. Kama wewe ni mtu wa furaha basi hiyo ndiyo funguo ya mafanikio yako.

Ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako ni muhimu kuzingatia Ishara hizo. Pandisha viwango vyako vya maisha, jifunze vipingamizi na kushindwa kama sehemu ya ukuaji wako, tengeneza mfumo wa watu walio tayari kuwa nyuma yako, usiwe mtu wa kulalamika, Kuwa na mambo ya kuangalia mbele, usijali watu wanavyokufikiria na mwisho ishi kwa furaha daima.

Weka email yako hapa na bonyeza NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.




Jiunge Kupata Makala hizi.

* indicates required


Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA