Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania.
Ni mara nyengine tena
tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina Imani kwamba utakuwa
unapata maarifa ya kutosha. Leo hii nimefanikiwa kukeletea Makala inayohusu
changamoto zinazoweza kukupatia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Katika maisha watu wengi
hawapendi kujihusisha na mambo ambayo yanawapa changamoto. Yapo mambo
ambayo binaadamu mara nyingi tunakuwa wazito kuyafanya. Tunashindwa kuyafanya
kwa sababu ya kuhofia usumbufu unaoweza kujitokeza. Uvivu unachangia kwa
asilima kubwa kushindwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuleta mafanikio. Ukweli
ni kwamba mambo yanayotupa changamoto kwenye akili zetu tukiweza kuyafanya
ndiyo yanayo tuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
Hizi hapa ndio changamoto ambazo
ukiweza kuzitatua zinaweza kukupatia mafanikio makubwa:
1.
Fanya Mambo Yaliyoshindikana
Ni kawaida kwa binaadamu kufanya
mambo ambayo ni rahisi kuyafanya. Binaadamu huwa hatupendi usumbufu. Unapoweza
kufanya mambo magumu yaliyoshindikana sio tu yanaweza kukuletea changamoto
lakini pia yataweza kukupeleka kufikia kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha
yako.
2.
Amka Mapema
Kuamka mapema unaweza kuiona
kama ni changamoto rahisi, lakini watu wengi tunakuwa wavivu wa kishindwa
kuamka mapema. Unapoweza kuamka mapema asubuhi itakusaidia kupata muda wa
kutosha kuweza kukamilisha kazi zako kwa wakati. Kuamka mapema kutakufanya
uweze kutengeneza mpango wa siku yako mzima, kuamka mapema kutakuwezesha
kufanya mazoezi, tahajudi na kuweza kuiweka akili sawa.
3.
Ongea Mbele za Watu
Changamoto kubwa inayowasumbua
watu wengi ni kushindwa kuongea mbele za watu. Kuweza kuongea mbele za watu
kunajenga uwezo wa kujiamini. Ili iwe rahisi kwako kuongea mbele za watu ni
muhimu kuchagua mada unayoifahamu na ambayo unaipenda.
4.
Sema Hapana
Unatakiwa kusema hapana kwenye
yale mambo ambayo hayana faida kwenye mipango yako. Unapoweza kusema hapana
utaruhusu kupata muda wa kutosha wa kufanya yale mambo ambayo yana ulazima
kwako. Hakikisha unatumia neno hapana kwenye mambo ambayo hayana msingi wowote
kwako.
5.
Usiahirishe mambo
Usipende kuwa na tabia ya
kuahirisha mambo. Kama kuna mambo ambayo ni muhimu kuyafanya hakikisha unafanya
na kuweza kukamilisha kwa muda muafaka. Usipende kuwa na tabia ya mazoeya ya
kusema nitafanya kesho kama unataka kuongeza thamani ya maisha
yako. Ni muhimu kuzingatia muda kwa kila jambo ulilopanga kulifanya na
hakikisha unalikamilisha.
Ili uweze kuboresha maisha yako
ni muhimu kuzingatia changamoto hizo. Fanya mambo yaliyoshindikana, hakikisha
unaweza kuamka mapema, ongea mbele za watu, jifunze kusema hapana na mwisho
acha tabia ya kuahirisha mambo.
Najua mambo haya yanaweza
kukupatia usumbufu kwa sababu umeamua kuanza tabia mpya ambayo hujaizoeya.
Lakini pia nakushauri usipende kufanya mambo kwa mazoeya.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena