Linapokuja suala la ufahamu wa pesa, watu wengi wanashindwa kujua maana halisi ya pesa.
Changamoto iliyopo kuhusu pesa
ni kwamba, wakati kila mtu anahitaji kupata pesa za kutosha za kuweza kutimiza
ndoto yake. Lakini hata unapoweza kuzipata pesa za kutosha utaona bado pesa
hazitoshi kukidhi mahitaji yake na kutimiza ndoto alizojiwekea. Pesa itaweza
kutosha pale utakapoweza kuiangalia kwa mtazamo tofauti.
Ni muhimu kutambua kwamba pesa
inahitaji mazingira mazuri ili iweze kustawi.
1.
Pesa Huweza Kufanya Mambo Kuwa
Mazuri
Unapokuwa na pesa ni lazima
uifanyie matumizi. Lazima ufikirie njia ya kuweza kuizalisha. Waswahili wana
msemo wanasema pesa ni sabuni ya roho. Pesa haiwezi kuwa na thamani kama
itabaki sehemu moja kwa muda mrefu. Fedha inapenda kuona mambo mapya. Inapenda
kuona inafanyiwa uwekezaji. Unapoweza kuiwekeza pesa ndivyo unavyoweza
kuiongezea thamani yake.
2.
Pesa Inahitaji Kuiwekea Lengo
maalumu
Umeshawahi kugundua kwamba, kama
kuna mahitaji unataka kununua, basi kwa mahitaji hayo utaona pesa inaonekana.
Lakini kama umejiwekea malengo maalumu kwa ajili ya pesa hiyo, utaona pesa
inakuwa ngumu kuipata. Hivyo tambua kwamba kama huna lengo maalumu kwenye akili
yako ni rahisi pesa kupotea. Na hii inapotea kwa sababu ni rahisi kufanya
matumizi yasiyo ya msingi. Matumizi mbayo hujayawekea malengo ni sawa na
kupoteza pesa ulioyoitafuta kwa muda mrefu.
3.
Pesa Inahitaji Malengo Ya Muda
Mrefu
Hili ni jambo muhimu ambalo mara
nyingi wanauchumi wanalizungumzia. Pesa ni lazima iwekewe mipango ya muda
mrefu. Moja ya sababu ambayo inatufanya tunakuwa na matumizi ya pesa ni
kutokana na kufanya matumizi tunapozipata pesa. Huwa tunapenda kufikiria
matumizi ya muda huo huo. Kufanya hivyo kunaathiri kutoyafikia malengo ya muda
mrefu.
4.
Pesa Zinapenda Kumfuata Mtu
Anayezipenda
Moja ya sifa kuu ya pesa ni
kwamba huwa zinakuwa na tabia ya kukimbilia kwa mtu anayezipenda. Kama
utashindwa kutambua matumizi sahihi ya pesa, basi fahamu kwamba zitamfuata mtu
mwenye kujua thamani ya pesa.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena