Jumamosi, 22 Oktoba 2016

Fahamu Mambo Manne ( 04 ) Yatakayo Kufanya Uweze Kuwa Na Mahusiano Mazuri Na Watu

 Karibu tena ndugu msomaji katika mfululizo wa makala zetu katika blogi yako uipendayo ya Nyota ya Mtanzania.

Katika Makala hii nitaendelea kuelezea  mambo mengine miongoni mwa mambo ambayo ukiyafanya yatakusaidia kujenga mahusiano mazuri katika jamii. Na unapojenga mahusiano hayo unakuwa umefungua milango ya mafanikio yako.

Haya hapa ndiyo mambo ambayo yanaweza kukujengea mahusiano mazuri na watu:

1. Wape Watu Nafasi Ya Kuongea
Unapotoa nafasi kwa watu ya kusikiliza na kuheshimu kile anachokiongea humfanya mtu huyo ajisikie amepewa heshima ya pekee. Kama unataka kujenga mahusiano mazuri na watu wengi ni muhimu kuwapa nafasi ya kuongea na wewe. Hakikisha unawapa muda wa kutosha wa kusikiliza maoni yao na mwisho wawekee mazingira ya kuthamini mchango wao.

2. Wafanye Watu Wajione Wana Thamani Ya Hali Ya Juu
Wafanye watu wajione wako juu. Usipende kabisa kuwadharau kwa mapungufu walionayo. Onesha ushirikiano na haki sawa kwa wote. Unapozungumza nao jenga tabia ya kuwaheshimu na kuwathamini. Tabia hii huwafanya wakuone una thamani kubwa kwao na hii itakufanya mahusiano yenu yachanue.

3. Usiwalaumu Watu Kama Kuna Tatizo Limetokea
Ni kawaida kwa watu wengi kutanguliza lawama mara tatizo linapotokea, kufanya hivyo mara nyingi tumeona kuvunjika kwa mahusiano. Kumbuka hakuna jambo linalovuruga upendo na mahusiano kama kulaumiana. Epuka kabisa kutumia lawama kama silaha yako kuu ya kuwahukumu watu wanapofanya makosa, badala yake ni vyema kutafuta chazo cha tatizo na kuangalia njia nzuri ya kutatua tatizo hilo pasipo na kuanza lawama. Hutoweza kudumu na ushirika mzuri wa mahusiano kama utatanguliza lawama.

4. Tuwapime Watu Kwa Mtazamo Chanya
Unapoamua kujenga mahusiano na watu hakisha unawapima kwa mtazamo chanya. Unapompima mtu kwa mtazamo hasi unamfanya ajisikie vibaya na kuhisi amedharauliwa, matokeo yake unakuwa umepunguza thamani ya mahusiano yenu. Ikitokea mtu huyo kuwa na mapungufu kwenye jambo lolote basi hakikisha unamueleza kwa lugha yenye kumsaidia aweze kurekebisha. Kufanya hivyo utamfanya ajisikie vizuri na kupelekea kudumisha mahusiano yenu.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA