Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Fahamu Mambo Mawili ( 02 ) Yatakayo Kufanya Uweze Kuwa Na Mahusiano Mazuri Na Watu


 Katika jamii tunayoishi tumezungukwa na watu tofauti tofauti. Wengine ni marafiki lakini pia wengine ni maadui zetu.  Mahusiano ni moja kati ya changamoto zinazotukabili katika maisha yetu ya kila siku. Wapo watu wanaoweza kukuunga mkono kwa mambo unayoyafanya lakini pia wapo wanaojenga chuki kwa hatua unazopitia.

Kipimo kizuri cha mafanikio ya maisha ni kuishi na watu vizuri. Unapoweza kuishi na watu vizuri utajenga tabia ya upendo kwa watu. Yapo mambo mengi mazuri tukiyafanya yanatupeleka kwenye kujenga mahusiano bora. Fahamu kwa kujenga mahusiano kwenye jamii ni jambo lenye maana sana kwa mafanikio yetu ya leo na kesho.

Katika Makala hii nitataja mambo mawili miongoni mwa mambo mengi ambayo ukiyafanya yatakusaidia kujenga mahusiano mazuri katika jamii. Na unapojenga mahusiano hayo unakuwa umefungua milango ya mafanikio yako.

1. Kubali tofauti zilizopo katika jamii
Tambua kwamba binadamu tunatafautiana kwa tabia. Tofauti zetu ni haki ya msingi kwa kila mtu. Hivyo unapoamua kujenga mahusiano na watu waliokuzunguka, usimuhukumu mtu kwa makosa anayofanya kutokana na kutofautiana kauli au mtazamo. Si lazima kupenda yale mambo wanayofanya wengine lakini tusijenge tabia za chuki kutokana na  yale wanayofanya wengine. Tusiruhusu akili zetu zipoteze muda kwa kufikiria kwamba ni kitu rahisi kuzifanya akili za wengine ziendane na vile unafikiria wewe. Ni kitu kisichowezekana  watu wote kuwa na tabia zinazofanana.

2. Jenga Tabia Na Mwenendo Utakaopendwa Na Watu
Binaadamu anatakiwa aishi kwa kuzingatia tabia na mwenendo wake mzima wa maisha. Tabia nzuri ndio msingi wa mafanikio ya kila mtu. Kumbuka tunatakiwa tutende wema, tuwe wacheshi, tuwe waadilifu ili tuweze kujenga mwenendo na kuonesha haiba nzuri ya tabia. Tengeneza mazingira yatakayoweza kujenga umoja na udugu kwa watu wako waliokuzunguka. Iwe ni kwenye kazi, majirani na hata watu unaoweza kukutana nao mara kwa mara. Kufanya hivyo kutakusaidia kujenga mahusiano mazuri na hali hiyo itakusaidia kufikia ndoto zako za mafanikio.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA